Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot afichua siri ya mkataba mpya Liverpool

SLOT Pict

Muktasari:

  • Liverpool kwa sasa ipo katika hatua nzuri ya kushinda taji la Ligi Kuu England ambapo kwa sasa ndio vinara, vilevile beki wao wa kati, Virgil van Dijk yupo katika hatua za mwisho kusaini mkataba mpya wakati Mohamed Salah tayari akiwa ameshasaini miaka miwili.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amefungua milango ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye kikosi hicho na kufunguka kwamba ameelewa kwanini kocha wa zamani wa timu hiyo Jurgen Klopp, alidumu kwa miaka minane Anfield.

Liverpool kwa sasa ipo katika hatua nzuri ya kushinda taji la Ligi Kuu England ambapo kwa sasa ndio vinara, vilevile beki wao wa kati, Virgil van Dijk yupo katika hatua za mwisho kusaini mkataba mpya wakati Mohamed Salah tayari akiwa ameshasaini miaka miwili.

Slot alisaini mkataba wa miaka mitatu katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kujiunga na majogoo hao wa Jiji la Liverpool akitokea Feyenoord.

Moja ya vitu ambavyo ameeleza vinawashawishi wachezaji na makocha kutamani kuendelea kuwa katika kikosi hicho ni furaha ambayo wamekuwa nayo, jambo ambalo hata yeye linamvutia.

"Sio matokeo pekee. Watu wanaofanya kazi hapa na mashabiki tulionao, nafikiri ndio wanaofanya timu hii kuwa ya kipekee, najua watu wa nje wanaangalia zaidi mabao tunayofunga au ushindi tunaopata. Lakini nafikiri ili kufurahia maisha yako ya kila siku, unahitaji kuwa na furaha unapokuwa kazini," alisema Slot.

"Hiyo ni moja ya sababu kwanini watu wanapenda kuwa hapa. Ndiyo sababu Jurgen alidumu kwa muda mrefu na kwa nini Mo amekubali kubaki kwa miaka miwili zaidi licha ya kuwa hapa kwa muda mrefu, ndiyo maana, kwa ujumla, wachezaji, makocha, na wafanyakazi wanabaki klabuni kwa muda mrefu.

"Tangu mwanzo nilipokewa vizuri na watu wa hapa wamekuwa wakishirikiana sana na mimi."

Slot yuko karibu kuwa kocha wa nne kushinda taji la Ligi Kuu ya England katika msimu wake wa kwanza, rekodi ambayo iliwahi kuwekwa na Jose Mourinho mwaka 2005, Antonio Conte mwaka 2017 wote wakiwa na Chelsea, Manuel Pellegrini mwaka 2014 akiwa na kikosi cha  Manchester City pamoja na Claudio Ranieri alipokuwa na Leicester City mwaka 2016.