Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sudan yaizuia Sudan Kusini Uwanja wa Ndege kwa saa 3

Muktasari:

Mchezo huo wa kundi B ambao Sudan itakuwa mwenyeji umepelekwa kuchezwa Libya kwasababu ya kukosa kiwanja kilichokidhi vigezo vya FIFA na CAF nchini mwao.

TIMU ya taifa ya mpira ya Sudan Kusini, 'Bright Stars', iliripotiwa kukwama kwenye uwanja wa ndege wa Benina huko Benghazi nchini Libya baada ya kuwasili kwaajili ya mchezo wa kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Sudan unaotarajiwa kupigwa Machi 25, saa 4:00 Usiku.

Mchezo huo wa kundi B ambao Sudan itakuwa mwenyeji umepelekwa kuchezwa Libya kwasababu ya kukosa kiwanja kilichokidhi vigezo vya FIFA na CAF nchini mwao.

Timu hiyo ilikwama kwa saa tatu kwenye uwanja huo wa ndege wakitajwa kutelekezwa na wenyeji wao Sudan.

Ripoti kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Sudan Kusini (SSFA) zilithibitisha kuwa timu ilikwama uwanja wa ndege kwa zaidi ya saa tatu kutokana na kutokuwapo kwa wawakilishi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Sudan, ambao walikuwa wanapaswa kuwakaribisha mara baada ya kuwasili.

Hali ilizidi kuwa mbaya wakati mamlaka za uhamiaji za Libya zilipochukua pasipoti za kusafiria za wachezaji na maafisa wa Sudan Kusini. Jambo hilo liliiacha timu katika hali ya kushindwa kuendelea na maandalizi yao kwa ajili ya mechi.

Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa X, SSFA ilichapisha picha na video zikionyesha Bright Stars kukwama kwenye chumba cha mapumziko cha uwanja wa ndege. Taarifa yao ilisomeka:

"Video ya Bright Stars wakikwama kwa saa tatu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Benina, Benghazi, Libya, wakati wawakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Sudan wakishindwa kufika kwa mapokezi yao huku pasipoti zikichukuliwa na Mamlaka ya Uhamiaji ya Libya.”

Licha ya changamoto hiyo, Bright Stars wanatarajiwa kuendelea na kampeni yao ya kufuzu Kombe la Dunia kicha ya usumbufu huo kuathiri ratiba na maandalizi yao kwa ajili ya mechi.


Msimamo Kundi B ulivyo

1.            Sudan – Pointi 11

2.            DR Congo – Pointi 10

3.            Senegal – Pointi 9

4.            Togo – pointi 4

5.            Mauritania- Pointi 2

6.            Sudan Kusini – Pointi 2