Tatum anavyoingia katika orodha ya matajiri NBA

Muktasari:
- Ni miongoni mwa mastaa waliosaini mikataba minono ya kuwafanya kuwa kati ya wanaoingiza pesa ndefu katika ligi hiyo na kuwapita baadhi ya mastaa na hii ni kutokana na kiwango chake kikubwa msimu huu akiichezea timu ya Boston Celtic.
BOSTON, MAREKANI: MOJA kati ya majina mapya katika orodha ya nyota wa Ligi ya Kikapu ya Marekani (NBA) wenye namba kubwa ni Jayson Tatum.
Ni miongoni mwa mastaa waliosaini mikataba minono ya kuwafanya kuwa kati ya wanaoingiza pesa ndefu katika ligi hiyo na kuwapita baadhi ya mastaa na hii ni kutokana na kiwango chake kikubwa msimu huu akiichezea timu ya Boston Celtic.
Licha ya mkwanja mrefu anaolipwa kutokana na mkataba huo wa miaka mitano, pia ana madili mengine yanayomfanya aishi kistaa na kampuni mbalimbali zinamtumia kujitangaza.

ANAPIGAJE PESA
Mkataba huo, kwa mujibu wa tovuti ya Spotracunamwingizia pesa ndefu na katika miaka hiyo mitano anatarajia kukusanya Dola 313 milioni na kila msimu anapata Dola 64 milioni.
Amesaini mikataba ya ubalozi na kampuni kama Jordan brand, Gatorade, Imo’s Pizza, NBA 2K and Subways, Fanatics, Google ,Hisense, Visual Technology, Netflix , New Era, Panini, PepsiCo na Ruffles na kwa mwaka inakadiriwa anapata zaidi ya Dola 20 milioni na kumfanya kuwa na utajiri wa Dola 80 milioni.
MJENGO
Jayson Tatum anamiliki nyumba ya kifahari yenye thamani ya Dola 4 milioni huko Newton, Massachusetts aliyoinunua mwaka 2019. Mjengoi huo unapatikana kwenye eneo lenye ukubwa wa futi 6,248 na ni ya ghorofa mbili inayojumuisha jiko la kisasa, sebule pana, chumba cha kulala.

NDINGA
2021 Rolls-Royce Wraith-Dola 343,350
Mercedes-AMG G 63-Dola 186,100
1968 Ford Mustang GT390-Dola 750,00

MSAADA KWA JAMII
Tatum ni mwanzilishi wa Jayson Tatum Foundation inayowasaidia vijana kwa mahitaji mbalimbali ili kutimiza ndoto zao ikiwamo msaada wa kimasomo. Taasisi hiyo inadhamini vijana kwenda katika kambi za kikapu za majira ya joto.
Mwishoni mwa mwaka 2017, Tatum na mpenzi wake Toriah Lachell walipata mtoto wa kiume aitwaye Jayson Jr jina lake la utani ni 'Deuce'.
Tatum ameonyesha mapenzi kwa mtoto wake kwa kutumia kiatu chenye jina lake. Tetesi zinadai, Tatum kwa sasa yupo katika uhusiano na Ella Mai baada ya kuachana na Lachell.