Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Thomas Partey, Jorginho wamvuruga kocha Arsenal

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Kuumia kwa wachezaji hawa kunazidisha hofu kwa mashabiki wa Arsenal kutokana na mchezo mgumu wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid uliopo mbele yao.

LONDON, ENGLAND: IKIWA ni siku kadhaa baada ya kupata ahueni juu ya hali ya majeruhi kwenye kikosi chake kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, tumbo limepata joto tena baada ya viungo wake, Thomas Partey na Jorginho kuumia katika mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Brentford jana Jumamosi.

Kuumia kwa wachezaji hawa kunazidisha hofu kwa mashabiki wa Arsenal kutokana na mchezo mgumu wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid uliopo mbele yao.

Partey alifunga bao la Arsenal katika kipindi cha pili, lakini alitolewa uwanjani katika dakika ya 69 baada ya kutojisikia vizuri na inaelezwa huenda asiwe sawa kucheza mechi ijayo dhidi ya Madrid.

"Hakuwa anajisikia vizuri, hivyo hatukutaka aendelee kucheza na kujihatarisha zaidi, hatujui kama atacheza Jumatano, bado sijazungumza na madaktari. Watamfanyia vipimo zaidi na kuona hali yake."

Arteta alikiri baada ya mechi kuwa alijua baadhi ya wachezaji wasingeweza kumaliza dakika 90, ingawa kutolewa kwa Partey haikuwa sehemu ya mpango wao.

"Tulikuwa na wazo hilo kwa sababu tunajua baadhi ya wachezaji wasingeweza kumaliza mechi. Hatukutarajia tatizo hilo kwa Thomas ingawa tulilazimika kumtoa."

Jorginho naye alitolewa akiwa anashika bega lake katika dakika za mwisho za mchezo huo, lakini Arsenal bado haijatoa taarifa kuhusu hali yake.

Mbali ya Partey ambaye alicheza vyema katika nafasi ya beki wa kulia na kufunga bao lake la nne msimu huu, mastaa wengine ambao wanatarajiwa kukosekana ni Ben White na Ricardo Calafiori.