Usiku wa hukumu Ligi ya Mabingwa Ulaya

Muktasari:
Aston Villa ambayo ina mlima mrefu wa kupanda dhidi ya PSG itakuwa nyumbani katika dimba la Villa Park kuikaribisha mabingwa hao wa Ufaransa.
MICHEZO ya kwanza ya mkondo wa pili hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kupigwa leo na kutakuwa na mechi mbili zote zikianza saa 4:00 usiku.
Aston Villa ambayo ina mlima mrefu wa kupanda dhidi ya PSG itakuwa nyumbani katika dimba la Villa Park kuikaribisha mabingwa hao wa Ufaransa.
Katika mchezo huo, Villa itatakiwa kushinda kwa ushindi wa kuanzia mabao 3-0 ili kwenda ingawa ikishinda 2-0 itatakiwa kucheza dakika 30 za ziada ambazo zikimalizika bila ya kupatikana mshindi basi mikwaju ya penalti itaamua.
Hii itakuwa ni mara ya pili kukutana kwa timu hizi tangu kuanzishwa kwao mara ya kwanza ikiwa ni ile mechi iliyopita na Villa ilichapwa mabao 3-1.
PSG inapambana kwa ajili ya kuchukua taji lao la kwanza katika historia ya michuano hii wakati Villa itakuwa inahitaji kuvuka ili kurudia historia yao ya msimu wa 1981/82 iliposhinda taji hili wakati huo likiitwa European Cup.
Mchezo mwingi kwa leo ni kati ya Borussia Dortmund na mimba ya Hispania, Barcelona ambao utakuwa na hisia za kipekee kwa Roberto Lewandowski kwa sababu atakuwa anarudi Signal Iduna Park mahali ambako alicheza kwa misimu minne kabla ya kuondoka kwenda Bayern Munich na baadae Barcelona.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza, Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, hivyo ili kupita, Dortmund itatakiwa kushinda 5-0 au irudishe hizo nne ili kwenda katika dakika za nyongeza.
Hii itakuwa ni mechi ya saba kwa timu hizi kukutana tangu mara ya kwanza msimu wa 1997/98 na zilicheza fainali iliyopigwa mara mbili ya kwanza Barca ikishinda 2-0 kisha ya pili ikamalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kesho, ndiyo kimbembe kwani Real Madrid itakuwa inacheza karata yao ya mwisho kujua ikiwa itatetea ubingwa wao au itaaga mashindano.
Madrid ikiwa nyumbani itakutana na Arsenal ambayo ina faida kubwa ya ushindi wa mabao 3-0 ilioupata katika dimba la Emirates wiki iliyopita.
Madrid itahitaji kushinda mabao 4-0 au kurudisha yale waliyofungwa Emirates ili kwenda katika dakika za ziada.
Mkubwa mwingine mwenye kazi ngumu ya kufanya ni Bayern Munich ambaye alichapika mabao 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Inter Milan, hivyo anahitaji kushinda mabao 2-0 ili kufuzu nusu fainali au ushindi wa 1-0 ili kwenda hatua ya dakika za nyongeza. Mechi hizi pia zinatarajiwa kupigwa kuanzia saa 4:00 usiku.