Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Hispania wakomaa kumngoa Cucurella Chelsea

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Klabu za Atletico Madrid, Barcelona na Real Madrid zinatajwa kuwa miongoni mwa zinazomuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye amekuwa nguzo muhimu katika eneo la ulinzi wa kushoto wa matajiri wa London, ambapo tangu msimu uliopita alikuwa akisakwa na timu kubwa Ulaya.

BEKI wa kushoto wa Chelsea na Hispania, Marc Cucurella, 27, huenda akarejea Hispania baada ya klabu kadhaa kuwasiliana na wawakilishi wake kuhusu uwezekano wa kumung'oa Stamford Bridge dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi.

Klabu za Atletico Madrid, Barcelona na Real Madrid zinatajwa kuwa miongoni mwa zinazomuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye amekuwa nguzo muhimu katika eneo la ulinzi wa kushoto wa matajiri wa London, ambapo tangu msimu uliopita alikuwa akisakwa na timu kubwa Ulaya.

Kutokana na hali ya sintofahamu inayoendelea katika kikosi cha Chelsea kuhusiana na msimu ujao ambapo hakitashiriki mashindano yoyote ya Ulaya, kuna uwezekano mkubwa wachezaji kadhaa wenye majina makubwa wakafirikia mustakabali wao, ikiwamo kusaka timu zingine zinazoshiriki michuano hiyo.

Cucurella alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walizungumza hadharani kutoridhishwa na uendeshaji wa Chelsea hasa baada ya kumfuta kazi Kocha Enzo Maresca mwanzoni mwa mwaka huu ambaye alitokea kuwa kipenzi cha mastaa wengi waliokuwa wakifurahishwa na uongozi wake. Nyota mwingine aliyeushutumu uongozi alikuwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Enzo Fernandez. Mkataba wa Cucurella ndani ya Chelsea unamalizika Juni 30, 2029.


Marco Palestra

NEWCASTLE United imemuweka beki wa kulia wa kimataifa wa Italia na Atalanta, Marco Palestra, kama chaguo la kwanza la usajili wa majira ya kiangazi yajayo kutokana na hofu ya kukimbiwa na nyota wake wa eneo hilo.

Hata hivyo, Newcastle United inaweza kukumbana na ushindani mkali kutoka kwa Manchester City, Arsenal na Inter Milan zinazofuatilia kwa karibu mustakabali wake katika kikosi chake cha sasa.

Palestra amekuwa bora katika eneo hilo akitoka kusugua benchi hadi kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza cha Atalanta. Mkataba wake unamalizika mwisho wa mwezi huu.


Pep Guardiola

MMILIKI mwenza wa Inter Miami, David Beckham, anadaiwa kutaka kumteua Pep Guardiola kuwa kocha wa klabu hiyo ya Ligi Kuu Marekani (MLS), baada ya kuondoka zake Manchester City mwishoni mwa msimu uliomalizika.

Hata hivyo, Guardiola anadaiwa kutokuwa tayari kurejea mara moja kwenye ukocha ikidaiwa kwamba anataka kupumzika kwa muda kushughulikia masuala yake binafsi kabla ya kuamua kurejea kazini.

Vyovyote iwavyo, kwa sasa kocha huyo atakuwa akishawishiwa na timu nyingi zitakazotaka kumwajiri kwa ajili ya kuzifundisha.


Bernardo Silva

KIUNGO wa kimataifa wa Ureno, Bernardo Silva, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Barcelona baada ya kuondoka Manchester City akiwa mchezaji huru mara tu baada ya kumalizika kwa msimu ulioisha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anataka dili hilo kukamilika kabla ya mwisho wa wiki hii, ambalo litamfanya kuwa usajili wa pili mkubwa katika kikosi hicho baada awali kumnyakua Anthony Gordon kutoka Newcastle United.


Marcus Rashford

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na England, Marcus Rashford, huenda akalazimika kurejea mazoezini Man United wakati wa maandalizi ya msimu mpya baada ya mpango wa kujiunga na Barcelona kukwama.

Manchester United inataka kuachana na Rashford ili kuongeza fedha za usajili kwa kocha wake mpya Michael Carrick anayetaka kuingiza wachezaji kadhaa katika kikosi hicho.

Timu za Arsenal, Chelsea, Newcastle United na Tottenham Hotspur zinafuatilia hali ya Rashford, lakini United haitaki kumuuza kwa mpinzani wake wa moja kwa moja katika Ligi Kuu England. Mkataba wake United unaisha Juni 30, 2028.


Ibrahim Sangare

NOTTINGHAM Forest inatarajiwa kufanya mazungumzo na kiungo wake wa kiamtaifa wa Ivory Coast, Ibrahim Sangare, kuhusu mkataba mpya huku Manchester United na Besiktas zikimfukuzia kwa karibu baada ya nyota huyo kudaiwa kuwa anataka kuondoka kikosini kutokana na kutofurahia maisha katika kikosi hicho, licha ya kujihakikishia namba.
 

Sangare amecheza mechi 28 Ligi Kuu England msimu uliomalizika, akifunga mabao mawili na asisti mbili huku Europa League akikipiga katika michezo 14. Mkataba anatarajia kuumalizika ifikapo Juni 30, 2028.


Hayden Hackney

KIUNGO wa kimataifa wa England na Middlesbrough, Hayden Hackney, 23, anawindwa na Manchester United inayopambana kuhakikisha kwamba inavuta mastaa wa maana kuziba pengo la Casemiro ambaye ameshaondoka katika kikosi hicho mara tu msimu wa Ligi Kuu England ulipomalizika wiki chache zilizopita.

Kocha wa Man United, Michael Carrick anamfahamu vizuri Hackney kutokana na kufanya naye kazi  alipokuwa akiifundisha Middlesbrough. Hata hivyo, huenda Mashetani Wekundu wa Old Trafford wakakumbana na wakati mgumu kumnasa kutokana na uwepo wa ofa nyingi mezani kwake dirisha hili la usajili.


Evann Guessand

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast, Evann Guessand, anatafakari mustakabali wake baada ya kifungu cha mkopo wake kutoka Aston Villa kwenda Crystal Palace cha kufanya usajili kuwa wa kudumu kumalizika muda wake mara tu baada ya kumalizika kwa msimu.

Guessand amekuwa na panda shuka katika ubora wake tangu alipotua Villa msimu dirisha lililopita kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda Palace ambako walau alipata nafasi ya kuonyesha ubora kwa miezi sita. Mkataba wake Villa unamalizika Juni 30, 2030.