Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Bongo wazitosa video kama Lil Wayne tu!

Muktasari:

  • Ipo hivi, kuna wanamuziki ambao walishirikishwa katika nyimbo za wenzao lakini katika video ya nyimbo hizo hawakuonekana kutokana na sababu zinazotofautiana. Fahamu zaidi.

Kama ambavyo Lil Wayne hakuonekana katika video ya wimbo wa Jennifer Lopez (J.Lo), I'm Into You (2011), ndivyo hivyo baadhi ya wanamuziki Bongo walivyofanya kwa wenzao waliowashirikisha.

Ipo hivi, kuna wanamuziki ambao walishirikishwa katika nyimbo za wenzao lakini katika video ya nyimbo hizo hawakuonekana kutokana na sababu zinazotofautiana. Fahamu zaidi.


1. Young Lunya: Rapa huyu hajaonekana katika video ya wimbo wa Q Chief, Mgodi (2026) ambayo imetoka hivi karibuni, ikiwa ni moja ya ngoma za EP yake mpya, Timeless.


2. Ruby: Mwimbaji huyu ambaye ametangaza kuachana na Bongofleva, hakutokea katika video ya ngoma ya Motra The Future, One Day (2016), na ile ya kundi la Yamoto Band, Su (2016).


3. Mr. Blue: Rapa huyo hakuonekana kwenye video ya wimbo wa mshiriki wa Tusker Project Fame 2007/08, Hemedy Phd, Rest of My Life (2015) ambao alichana vizuri tu.


4. Marioo: Hakutokea katika video ya Nandy, Tonge Nyama (2025), lakini pia video hiyo ilikuja kuondolewa YouTube kutokana na mgogoro wa hakimiliki ambapo Nandy alituhumiwa kuiba wimbo huo.


5. Belle 9: Mwimbaji huyu kutokea Morogoro hakuonekana kwenye video ya wimbo wa Young Killer na Fid Q, 13 (2014), pia video ya Edu Boy na Amber Lulu, Tunasafisha (2018). Hata hivyo, awali tayari Belle 9 alikuwa ameshatokea kwenye video nyingine za nyimbo za wasanii hao ambazo ni Dear Gambe - 2013 (Young Killer), na Yes or Now - 2015 (Edu Boy).


6. Appy: Ameshiriki katika wimbo mpya wa Jux na Stonebwoy, Sexy & Bad (2026) ila kwenye video hajaonekana wala kutajwa kama alishirikishwa, hatua ambayo imefanya kulalamikia jambo hilo.


7. Chid Benzi: Kipindi yupo juu sana kimuziki alishirikishwa na Lady Jaydee katika wimbo wake, Upo Juu (2009) ila kwenye video hakuonekana kitu kilichopelekea vesi yake kufutwa!.


8. Rich Mavoko: Wakati bado yupo chini ya usimamizi wa WCB Wasafi, ndipo hakutokea katika video ya wimbo wa TID, We Dada (2018).


9. Nikki wa Pili: Rapa huyu kutokea kundi la Weusi, hakuonekana katika video ya mwanamuziki aliyeibuliwa na Tanzania House of Talent (THT), Pipi, Hafai (2016).


10. Jux: kipindi akifanya vizuri zaidi katika miondoko ya RnB, Jux alipewa kolobo nyingi sana na wasanii wa rap lakini mwisho wa siku hakutokea katika video tatu za ngoma hizo. Video hizo ni za wasanii kama Mabeste (Sirudi Tena - 2012), Lord Eyes (Hela Yangu - 2017), na Mtu Chee (Mtu Tatu - 2015). Ikumbukwe Mtu Chee lilikuwa ni kundi liloundwa na Stamina, Country Wizzy na Young Killer.