Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzee Yusuf ataja sababu kukosa shoo ya Isha Mashauzi

MZEE Pict

Muktasari:

  • Maswali hayo yalitokana na historia ya uhusiano wao katika muziki wa Taarab, ikizingatiwa kuwa Mzee Yusuf ni miongoni mwa watu waliochangia safari ya Isha, hasa wakati alipokuwa akifanya kazi katika bendi ya Jahazi Modern Taarab iliyokuwa chini ya uongozi wake.

KUTOKUWEPO kwa mkongwe wa muziki wa Taarab, Mzee Yusuf, katika shoo ya kusherehekea miaka 20 ya Isha Mashauzi kwenye muziki iliyofanyika Jumamosi, Oktoba 24, 2026, kumeibua maswali kwa baadhi ya mashabiki na wadau wa muziki huo.

Maswali hayo yalitokana na historia ya uhusiano wao katika muziki wa Taarab, ikizingatiwa kuwa Mzee Yusuf ni miongoni mwa watu waliochangia safari ya Isha, hasa wakati alipokuwa akifanya kazi katika bendi ya Jahazi Modern Taarab iliyokuwa chini ya uongozi wake.

Kutokana na hilo, Mzee Yusuf ameliambia Mwanaspoti kuhusu sababu iliyomfanya ashindwe kuhudhuria shoo hiyo, akisema alikuwa na majukumu mengine ya kimuziki.

MZE 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Mzee Yusuf amesema, Isha alikuwa ana taarifa kwamba hataweza kufika kutokana na kuwa na shoo ya harusi siku hiyo, ndiyo maana alimwambia mkewe, Leyla Rashid, ahudhurie kwa niaba yake.

“Mimi wala sina tatizo na Isha, yule ni mwanangu na hatujawahi kuwa na tatizo naye, mbona ameshafanya matamasha kama mawili hivi na amenialika nikahuduria, sema hii ya sasa hivi nilikuwa na kazi ya harusi siku hiyo, na Isha anajua kwa sababu nilimweleza mapema, ndiyo maana nilimwambia mke wangu Leyla,” amesema Mzee Yusuf.

MZE 02

Mzee Yusuf amebainisha kwamba, baada ya shoo kumalizika, Isha alimpigia simu na kumjulisha kuwa alikuwa amemaliza shughuli hiyo, huku akimshukuru.

Kwa upande wake, Isha Mashauzi alipozungumza na Mwanaspoti kuhusu kutokuwepo kwa Mzee Yusuf katika shoo hiyo, alisema alimjulisha mkongwe huyo kuhusu maadhimisho hayo, lakini alielezwa kwamba alikuwa na kazi nyingine siku hiyo.

"Mzee nilimualika ila alikuwa na kazi ya shoo ndio maana ameshindwa kufika hapa, ila nashukuru amenipa thamani ya kumwambia mke wake Leyla aje kwenye shoo na kuacha kazi ya bendi," amesema.

MZE 03

Safari ya Isha Mashauzi katika muziki wa Taarab inahusishwa na bendi ya Jahazi Modern Taarab, iliyokuwa chini ya uongozi wa Mzee Yusuf, ambako alipata nafasi ya kujifunza na kuimarisha uwezo wake katika muziki huo.

Isha alijiunga na Jahazi Modern Taarab mwishoni mwa mwaka 2007. Katika hatua ya mwanzo ya safari hiyo, Isha alipata nafasi ya kupanda jukwaani na bendi hiyo, akiimba wimbo wa Hayanifiki, uliotungwa na Mzee Yusuf. Wimbo huo ulitajwa kuwa miongoni mwa nyimbo zilizomsaidia Isha kutambulika zaidi katika muziki wa Taarab.

Baadaye, Isha aliendelea kujijengea jina katika tasnia hiyo na kufikia hatua ya kuanzisha bendi yake ya Mashauzi Classic mwaka 2011, akiwa pamoja na Thabit Abdul.

Historia hiyo inaonyesha kwa nini Mzee Yusuf anatajwa miongoni mwa watu waliohusika katika safari ya Isha ya muziki, na kwa nini kutokuwepo kwake katika maadhimisho ya miaka 20 kulizua maswali kwa baadhi ya mashabiki.