Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakongwe Bongo Fleva wanaotikisa Gen Z

WAKONGWE Pict

Muktasari:

  • Kitu kikubwa kinachowabeba wakongwe hao ni ujumbe ambao unaishi muda wote katika jamii, ukiachana na hilo aina ya midundo iliyotumika kwa baadhi ya nyimbo zao inachezeka.

WAPO baadhi ya wasanii wakongwe wa Bongo Fleva ambao wakipanda jukwaani, wana ushawishi mkubwa mbele ya kizazi cha Gen Z ambacho hakipendi mambo magumu.

Mwanaspoti linakuchambulia baadhi ya wasanii hao, waliyo na ushawishi mkubwa kwa rika zote na nyimbo zao wanapopafomu zinakuwa na muitikio mkubwa na mashabiki zao.

Kitu kikubwa kinachowabeba wakongwe hao ni ujumbe ambao unaishi muda wote katika jamii, ukiachana na hilo aina ya midundo iliyotumika kwa baadhi ya nyimbo zao inachezeka.

WAKON 04

Abbas Hamisi Kinzasa ‘20 Percent’

Japokuwa 20 Percent siyo mtu anayependa sana kucheza, lakini asilimia kubwa ya midundo iliyotumika kwenye nyimbo zake inachezeka na anaweza akaamsha vaibu jukwaani kama Tamaa Mbaya, Ya Nini Malumbano, Money Money na ni kati ya wakongwe wanaoonekana wanakubalika sana kwenye mitandao ya kijamii.

Kitu ambacho hakijawahi kutoka kwenye maisha ya mashabiki wake ni ubunifu wake aliowahi kuufanya, nyimbo zake kama Mama Neema kuubadilisha kuufanyia filamu, uhalisia walioonyesha waigizaji ulivuta hisia za watu wengi, laiti zingekuwa katika mfumo wa kidijitali basi huenda wengi wangekuwa wanaufuatilia hadi sasa.

Staa huyo aliyewahi kunyakua tuzo tano kwa mpigo za Kili Music Awards, kipindi cha nyuma Mwanaspoti liliwahi kumtembelea nyumbani kwake Kimanzichana lilishuhudia namna ambavyo wakazi wa eneo hilo wanavyomkubali na kumpa heshima yake na anavyoishi maisha halisi.

Bado anaendelea kutoa ngoma kali zinazomfanya aendelee kufuatiliwa zaidi na rika zote, miongoni mwa hizo ni Nipeleke kwa Mama, Nyumba Ya Milele aliyomshirikisha EBL Ebl DRuCuLa, wimbo huo ulipokelewa kwa ukubwa kutokana na ujumbe wake, unaokumbusha kifo.

20 Percent aliwahi kusema: “Uandishi wangu ni ule unaoishi, sina presha ya kukimbizana kutoa nyimbo ambazo haziwezi kuwa na tija kwa jamii, mfano Mali za Urithi ni vitu ambavyo vinaishi kwenye jamii.”

WAKON 05

Juma Kassim ‘Sir Nature’

Sauti yake ni ile ile hadi sasa, nyimbo zake nyingi zilikuwa za kuchezeka kama Hakuna Kulala, Mtoto Iddi, Staki Demu.

Jina la Nature bado linaendelea kusikika kwenye masikio ya mashabiki wa muziki nchini.

Siyo msanii ambaye anatoa ngoma mara kwa mara, lakini anasikika mara kwa mara kwenye mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari nchini, jambo ambalo linafanya afuatiliwe na Gen Z.

Sir Nature aliwahi kusema: “Muziki wa sasa vijana wengi wanalipua lipua, mfano kuna nyimbo zinatakiwa kupigwa usiku, ila zinapigwa mchana na hazipaswi kusikilizwa na watoto, hilo linapaswa kukemewa ili wasanii tuendelee kuwa kioo cha jamii.”


Lucas Mkenda ‘Mr Nice’

Nyimbo zinazochezeka ni kama Fagilia, Kikulacho ambao ujumbe wake bado unaishi, kulingana na usaliti unaoendelea katika maisha ya watu.

Hivi karibuni katika miaka 30 ya Bongo Fleva, baada ya kupanda jukwaani shangwe liliibuka kwa mashabiki wake, hasikiki sana kwa sababu maisha yake muda mwingi anaishi nchini Kenya.


Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’

Rapa wa muziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ ambaye serikalini cheo chake ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, bado akipanda jukwaani anakiwasha.

Bado nyimbo zake zipo kwenye chati na zinapendwa na vijana wengi kama We Endelea Tu, Kiboko Yangu aliyoshirikiana na Ali Kiba.

Mwana FA bado anaendelea kufanya kolabo na wasanii mbalimbali mfano wimbo wa Sio Kwa Ubaya alioufanya na Maua Sama na Harmonize, ukiacha hilo ni mtu anayefanya sana mazoezi jambo linalompa pumzi anapoimba bado anaonekana ni yule yule.

WAKON 01

Dully Sykes

Miongoni mwa nyimbo zake akiamua kukiwasha jukwaani kwa pumzi ya mazoezi ya kutosha anaweza akakiwasha ni kama Kupenda, Hunifahamu, Hai zinachezeka, hivyo anaweza akateka hisia za mashabiki ambao ni Gen Z.

Jambo lingine linalomfanya aendelee kuwa na ushawishi kwa mashabiki wake ni kuendelea kufanya kolabo na wasanii mbalimbali wa sasa mfano wimbo wa King&Queens aliyomshirikisha Zee Cute, video yake ni kilekile wanachopenda kuona Gen Z, ukiachana na hilo bado anavaa kistaa hajakubali kubaki nyuma.

WAKON 02

Feruzi Mrisho Rehan ‘Ferooz’

Miongoni mwa nyimbo zake kali hata akipanda jukwaani na ziliwahi kuvuta hisia za watu hadi sasa ina ushawishi ni Starehe aliyoshirikiana na Professor Jay, huku baadhi ya mashabiki waliamini kama kweli ana ngoma, kumbe alibeba uhalisia.

Kupitia wimbo huo, aliwahi kusema kuna baadhi ya mashabiki waliamini ana maambukizi ya UKIMWI: “Ni wimbo niliouimba kwa hisia kali, ambazo ziliwafanya mashabiki waamini nilikuwa mtu wa starehe na nina ngoma, siyo kweli niliamua kuvaa uhalisia.”

Mbali na hilo Ferooz ni msanii aliyemaintain muonekano wake, hivyo bado ana uwezo wa kulimiliki jukwaa na kucheza pamoja na mashabiki kwa muda mrefu.

WAKON 03

Rashidi Abdallah Mohamed ‘Chidbenz’

Mwana Hip Hop ni kati ya wasanii ambao akipanda jukwaani na kuimba mashabiki wanakuwa na mwitikio wa nyimbo zake, Dar es Salaam Standup.

Ingawa kwenye kucheza haijawa kama zamani, ana mabadiliko makubwa ya muonekano wake, lakini hilo haliondoi anapopanda jukwaani kupata shangwe za mashabiki wake, nje ya mikasa ya hapa na pale aliyowahi kupitia, Chidbenz anafuatiliwa zaidi na mashabiki kutokana na misimamo yake na majibu anayotoa akiwa anahojiwa, miongoni mwa hayo aliwahi kuulizwa amewaandalia nini mashabiki wake wakaji akijiandaa kupanda jukwaani alijibu atapika wali baadaye.


Rehema Chalamila ‘Ray C’

Tangu zamani alikuwa ana vaibu la kuimba na kucheza kwa kunengua kiuno kama wanavyofanya baadhi ya wasanii wa sasa, miongoni mwa nyimbo zake zinazoweza kuchezeka ni Wanifuatia Nini, Unanimaliza, Mama Ntilie.

Katika mtandao wa TikTok mabinti wengi wamekuwa wakifanya chalenji za nyimbo zake, mfano Wanifuatia Nini wengi wao wakionyesha maumivu ya kutendwa kimahusiano.