Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EBANA EE! Slot aliitwa Miss sasa maisha hayoo

SLOT Pict

Muktasari:

  • Pointi moja tu dhidi ya Tottenham siku ya Jumapili ndio itamfanya kuwa kocha wa kwanza kutoka Uholanzi kushinda taji hilo. Lakini huyu Slot ni nani? shuka naye hapa.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot anahitaji dakika 90 tu zijazo kuiongoza Liverpool kutwaa taji la 20 huku akiwa katika msimu wake wa kwanza kama kocha mkuu wa majogoo hao.

Pointi moja tu dhidi ya Tottenham siku ya Jumapili ndio itamfanya kuwa kocha wa kwanza kutoka Uholanzi kushinda taji hilo. Lakini huyu Slot ni nani? shuka naye hapa.

Slot alizaliwa katika kijiji kidogo cha Bergentheim, Uholanzi mwaka...Katika siku zake za awali kama mchezaji, Arne alipewa jina la utani “Miss Slot” lililoibuka kutokana na tabia yake ya kutopenda mazoezi, mvivu na mtu aliyekuwa mpole na muda wote alipokuwa uwanjani hakuwa anataka hata kuchafua jezi yake.

Kocha wa FC Zwolle wakati huo, Jan Everse, alikuwa mmoja wa watu muhimu zaidi katika maisha ya mwanzo ya Slot na anaeleza kwamba  uhusiano wao haukuanza vizuri.

SL 01

Everse, ambaye sasa ana umri wa miaka 71, aliambia SunSport:

“Hakuna ambaye angeweza kupiga pasi bora kama  Arne.

Lakini kimwili, hakuwa mwepesi. Namna alivyokimbia, alikuwa ni mvivu.

Kama hali ya hewa ilikuwa mbaya na uwanja umejaa tope, bado ungeweza kuona  jezi yake bado iko safi. Ungeweza kuiweka moja kwa moja kabatini bila hata kuifua baada ya mechi kumalizika.

Ilikuwa ukimpa mpira, mara nyingi sana alifanya kitu kizuri, lakini nilikuwa mkweli kwake. Nilimwambia, ‘Arne, wewe ni mmoja wa wachezaji wangu bora, lakini tatizo lako ni kwamba hujitoi vyakutosha. Unahitaji kufanya kazi kubwa sana kwenye kiwango chako cha mazoezi ya mwili. Ulivyo ni rahisi sana kupitika."

SL 02

Everse alimuita kiungo huyo mshambuliaji wa miaka 17 kwa wakati huo “Juffrouw Slot" likimaanisha “Miss Slot” kutokana na jinsi alivyocheza.

"Baada ya kumwambia vile ilibidi aanze mazoezi, mwanzoni hatukuwa na uhusiano mzuri kwa sababu hakuwa anapata nafasi ya kucheza. Hivyo alikuwa na hasira nami  lakini alikuwa na akili ya kuelewa sababu iliyomfanya asicheze, nina uhakika nilibadilisha mtazamo wa Arne kuhusu jinsi ya kuwa mchezaji wa mpira."

Hata hivyo, Slot alibadilisha mtindo wake wa maisha baada ya kuumia na kukaa nje kwa karibia mwaka mmoja, akiwa majeruhi alifanya sana mazoezi na aliporejea haraka akawa sehemu ya kikosi cha kwanza.

SL 03

SAFARI YAKE

Wakazi wa kijiji alikozaliwa Slot watakuwa wamekita macho kwenye runinga Jumapili, wakitarajia kushuhudia historia ikiandikwa.

Kijiji cha Bergentheim, chenye wakazi 3,500, kiko kando ya reli ya Emmen-Zwolle na katikati yake umepita   mfereji.

Kina makanisa mawili, duka moja kubwa, shule chache za msingi, na inapatikana timu ya soka ya VV Bergentheim, ambako Slot alijifunza kucheza mpira miaka ya 80.

Alikuwa akitembea umbali wa karibu kilomita moja hadi uwanja wa Sportpark Moscou kupitia daraja pekee kijijini, na alicheza hapo hadi alipoonekana na maskauti wa Zwolle akiwa na umri wa miaka 12.

Baba Slot ambaye ni Mwalimu mkuu wa zamani, ambaye alizingatiwa kuwa mchezaji bora zaidi kuliko mwanawe, alikuwa mchezaji wa timu ya ridhaa ya Uholanzi iliyokaribia kufuzu kwa Olimpiki za Montreal mwaka 1976.

Siku hizi, Slot Sr hutazama mechi za Liverpool kwenye televisheni na ni mwanachama wa heshima wa VV Bergentheim.

SL 04

Bert Nijenhuis, mwenye miaka 66, amekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kwa miaka saba na alicheza pamoja na baba yake Slot, Arend miongo iliyopita katika mahojiano na The Sun anasema:"Sisi sote tunajivunia sana mtoto wa Arend. Arne ni mwerevu, ana maarifa, ni hodari  na ana  uelewa mkubwa wa mpira wa miguu. Ana nidhamu, bidii ya kazi na huendeleza wachezaji. Huwapa nafasi wafanye kile wanachokiweza. Baba yake ndiye kocha wake wa kwanza. Tunaeshimu sana kwa kile anachokifanya sasa."

Baadhi ya wakazi wa kijiji chake wamependekeza kujengwa sanamu kwa heshima ya kocha huyu pindi atakapotwaa rasmi taji  la Ligi Kuu.

Kocha wa zamani wa Slot, Everse, ambaye alikuwa beki wa kushoto wa Feyenoord na Ajax hadi jeraha lilipokatiza maisha yake ya soka, anadai aliamini kwamba Slot angefanikiwa zaidi kwenye soka la England kuliko mtangulizi wake Erik ten Hag  ambaye alifukuzwa na Manchester United Oktoba baada ya kushindwa kuirejesha timu hiyo kwenye mafanikio ya Ligi Kuu.

Everse alisema: “Arne ni mwerevu, huhesabu hadi kumi kabla hajazungumza. Anajua haswa la kusema.”

Hata hivyo, Slot alifukuzwa uwanjani, akafungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya Pauni 70,000 baada ya kumkemea mwamuzi Michael Oliver kwa maneno makali kufuatia sare ya 2-2  dhidi ya Everton,  Februari mwaka huu.

SL 05

FA ilifichua kuwa Slot alimshutumu Oliver kwa "kuwapendelea wapinzani wao kwa kila kitu" kabla ya kusema kwa hasira:

"Tukikosa ubingwa, nitakulaumu wewe!"

Nijenhuis alikiri: "Huo ndio wakati pekee ambapo hisia zilimshinda. Lakini hiyo si tabia ya Arne. Yeye huwa mtulivu kila mara."

Everse aliongeza: "Ana falsafa nzuri ya soka. Najua kwa sababu ilikuwa falsafa yangu.

Lazima uwaandae wachezaji kwa kila jambo kabla ya mechi ili wasikumbwe na mshangao wowote.

Lazima ufundishe akili zao kwa sababu mpira unachezwa kwa kichwa."

Mtindo wa kufundisha wa Slot uliimarika alipokuwa msaidizi kwenye timu za Cambuur na AZ Alkmaar ambako walimaliza wa pili nyuma ya Ajax kati ya 2016 na 2020.

Aliwaongoza miamba ya Uholanzi Feyenoord kufika fainali ya Conference League ya 2022 (ambayo walifungwa na Roma ya Jose Mourinho) na kisha kushinda taji la Eredivisie 2023, akivunja utawala wa Ajax nchini humo hali iliyoivutia sana Liverpool.

Everse alitabiri kwamba Slot atakuwa na mafanikio ingawa alikuwa anachukua nafasi ya Jurgen Klopp.

"Mwanzoni mwa msimu, nilisema, ‘Yeye ni kocha bora kuliko Klopp."

Wakati mwingine, Slot ambaye ana watoto wawili Joep na Isa aliozaa na mkewe Mirjam  anapokwenda kijijini kwao kuwatembelea wazazi wake, huwa anapitia katika akademi aliyokulia  ya VV Bergentheim ambapo hutenga muda na kuwafundisha watoto.