Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauzo ya kihistoria EPL: Ronaldo juu, Isak nje ya kumi bora

MAUZO Pict

Muktasari:

  • Majira haya ya kiangazi yameshuhudia Morgan Rogers, Elliot Anderson na Sandro Tonali wakihusika katika dili za zaidi ya pauni100 milioni, lakini utafiti wa Valuball unaonyesha kuwa thamani halisi ya baadhi ya usajili wa zamani ni kubwa zaidi kwa viwango vya sasa.

LONDON, ENGLAND: LICHA ya dirisha hili la usajili kushuhudia wachezaji watatu wa Ligi Kuu England kuuzwa kwa zaidi ya pauni100 milioni kila mmoja, hakuna hata mmoja anayekaribia rekodi ya Cristiano Ronaldo baada ya thamani za usajili huo kurekebishwa kulingana na mfumuko wa bei.

Majira haya ya kiangazi yameshuhudia Morgan Rogers, Elliot Anderson na Sandro Tonali wakihusika katika dili za zaidi ya pauni100 milioni, lakini utafiti wa Valuball unaonyesha kuwa thamani halisi ya baadhi ya usajili wa zamani ni kubwa zaidi kwa viwango vya sasa.

Cristiano Ronaldo ndiye anayeongoza orodha hiyo baada ya kuondoka Manchester United na kujiunga na Real Madrid mwaka 2009 kwa pauni 80 milioni. Kwa kuzingatia mfumuko wa bei, dili hilo lingekuwa na thamani ya takribani pauni292 milioni leo, karibu mara tatu ya thamani ya usajili wa Tonali kutoka Newcastle kwenda Tottenham.

MAU 01

Nafasi ya pili inashikiliwa na Eden Hazard aliyesajiliwa na Real Madrid kutoka Chelsea mwaka 2019. Ingawa Real ililipa hadi pauni150 milioni  baada ya bonasi mbalimbali kutimia, thamani ya dili hilo kwa viwango vya sasa imefikia pauni245 milioni. Hata hivyo, Hazard alishindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa kutokana na majeraha yaliyomkumba mara kwa mara.

Alan Shearer anafunga tatu bora kupitia uhamisho wake kutoka Blackburn Rovers kwenda Newcastle United mwaka 1996. Wakati huo dili hilo lilikuwa la pauni15 milioni, lakini leo lingekuwa na thamani ya pauni238 milioni.

MAU 02

Real Madrid inaendelea kutawala orodha hiyo kupitia usajili wa Nicolas Anelka kutoka Arsenal mwaka 1999. Ada ya pauni23.5 milioni  iliyolipwa wakati huo sasa ingekuwa sawa na pauni226 milioni.

Philippe Coutinho naye anaingia kwenye orodha baada ya kuondoka Liverpool kwenda Barcelona mwaka 2017 kwa pauni142 milioni. Kwa thamani ya sasa, usajili huo ungefikia pauni217 milioni, huku fedha hizo zikisaidia Liverpool kujenga kikosi kilichokuja kutwaa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya Jurgen Klopp.

MAU 03

Paul Gascoigne anashika nafasi ya sita baada ya kuhamia Lazio kutoka Tottenham mwaka 1992 kwa pauni5.5 milioni, dili ambalo leo lingekuwa na thamani ya pauni 197milioni.

Arsenal inaonekana tena kupitia Marc Overmars aliyesajiliwa na Real Madrid mwaka 2000 kwa pauni25 milioni. Kwa viwango vya sasa, usajili huo ungegharimu pauni196 milioni, jambo ambalo lingeifanya Arsenal kuvuna zaidi ya pauni 400milioni kutokana na mauzo mawili kwa miamba hiyo ya Hispania.

MAU 04

Gareth Bale, aliyesajiliwa na Real Madrid kutoka Tottenham mwaka 2013 kwa pauni86 milioni, anashika nafasi ya nane, huku thamani ya dili hilo leo ikifikia pauni192 milioni.

Nafasi mbili za mwisho katika 10 bora zinakwenda kwa Stan Collymore na Rio Ferdinand. Collymore alitoka Nottingham Forest kwenda Liverpool mwaka 1995 kwa pauni8.5 milioni, ambazo kwa sasa zingekuwa na thamani ya pauni179 milioni.

MAU 05

Kwa upande wa Ferdinand, alihama Leeds United kwenda Manchester United mwaka 2002 kwa pauni30 milioni, rekodi ya Uingereza wakati huo. Leo, usajili huo ungekuwa na thamani ya takribani pauni 175milioni.

MAU 06

Cha kushangaza, usajili unaoshikilia rekodi halisi ya ada kubwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu England, ule wa Alexander Isak kujiunga na Liverpool kwa pauni 130 milioni msimu uliopita, unashika nafasi ya 24 pekee kwenye orodha hiyo baada ya thamani zake kurekebishwa kulingana na mfumuko wa bei.