Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 30 Bongofleva ingekuwa vipi Ligi Kuu Bara?

MIAKA 30 Pict
MIAKA 30 Pict


FAMILIA ya Bongofleva iko kwenye sherehe kubwa za miaka 30 ya muziki huu pendwa hapa nchini.


Miaka 30 siyo ya kugunduliwa kwa muziki huo, bali kugunduliwa kwa jina hilo. Ni kwamba Bongofleva asili yake ni muziki wa Kimarekani ulioingia kwa kishindo nchini na kuvutia vijana wengi kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1980 kuelekea miaka ya 1990.


Muziki huo hasa ulikuwa hip hop (rap) na ndiyo maana jina la kwanza kabisa lilikuwa Swahili Rap. Baadaye R&B ikaingia ndani yake na kuendelea kuvutia vijana. Lakini, wakati wote huo muziki huo haukuwa ukichezwa kwenye redio badala yake watu walisikilizishana mitaani mwao tu. Kulikuwa na sababu kubwa mbili:


MIAKA 04

1. LUGHA

Wasanii wa mwanzo kabisa waliimba kwa Kiingereza. Katika zama za miaka ya 1990 na kurudi nyuma Kiingereza kilikuwa anasa kubwa sana nchini. Tofauti na sasa ambapo watangazaji wa redio za Kiswahili wanachanganya maneno mengi ya Kiingereza, wakati ule redio ilikuwa moja tu, Redio Tanzania Dar es Salaam na haitumii hata neno moja la Kiingereza.

Kwa hiyo msanii wa Kitanzania, tena wa kizazi kipya, muziki ambao bado ulikuwa wa kihuni asingepata nafasi kwa kutumia Kiingereza.


MIAKA 05

2. HAKIMILIKI

Baadaye wakaanza kuimba kwa kama alivyofanya Saleh Jabir, mshindi wa mashindano ya Yo! Rap Bonanza 1991. Lakini, hata hawakuwa Wakiimba nyimbo zao binafsi.  Walichofanya ni kupita kwenye nyimbo zilezile za wasanii wa Ulaya na Marekani na kutungia mashairi ya Kiswahili juu yake, na kuimba kwa kutumia mtiririko na mdundo uleule.

Saleh Jabir alifanya hivyo kwenye OPP ya Naughty by Nature na hata Ice Ice Baby ya Vanilla Ice. Nyimbo kama hizo kuzicheza redioni ni kesi kutokana na hakimiliki.


MAPINDUZI

Baadaye ndiyo wakaja kina Joseph Mbilinyi aka 2Proud au Sugu kwa sasa, na kuanza kutunga nyimbo zao wenyewe kwa kutumia midundo yao.

Hapo ndipo muziki huu ukaanza kupata sura mpya na kuanza kupigwa redioni.

Redio hiyo ilikuwa Radio One Stereo kupitia kipindi cha DJ Show cha Taji Liundi na Mike Mhagama. Walianza kupiga muziki huo redioni mwaka 1994, wakitumia jina la Swahili Rap. Hata hivyo, haikuwa rahisi. Sera za redio hazikuruhusu nyimbo hizo kupigwa, lakini vijana hawa wawili walilazimisha.

Walianza na wimbo wa NI MIMI wa 2Proud ambao ukawemo kwenye albamu yake ya 1995 yenye jina hilo hilo. Mkubwa wao wa kazi, Julius Nyaisanga ‘Uncle J’ ambaye sasa ni marehemu, akiwa mtaani akasikia muziki wa kizazi kipya unapigwa redioni. Akashuka na kuwasha gari hadi studio ili akawafundishe adabu. Hadi anafika wimbo umeisha na alichokikuta kikamshangaza.

Studio ilikuwa ‘bize’ kupokea simu za wasikilizaji wakiomba wimbo urudiwe. Hapo akaamini kwamba kumbe mtaa unapenda hizi nyimbo, akaruhusu. Taji Liundi na Mike wakaendelea kupiga Swahili Rap hadi 1996 ndio wakaja na jina jipya la BongoFleva 1996.

Kwa hiyo sherehe za miaka 30 ya Bongofleva ni kuanzia 1996 pale jina lilipoanza, sio muziki wenyewe kuanza. Muziki ulianza nyumba ya hapo.


MIAKA 02

INGEKUWA VIPI KWENYE LIGI?

Mwaka mmoja baada ya kuanzishwa jina la BongoFleva, mapinduzi mengine makubwa yakaja kwenye mpira wetu. Mwaka 1997 ligi ya Tanzania Bara ilijipandisha hadhi na kuwa Ligi Kuu kutoka Ligi Daraja la Kwanza kama ngazi ya juu kabisa.

Kabla ya hapo, Tanzania Bara kulikuwa na madaraja manne ya ligi yaliyoanza mwaka 1982; Ligi Daraja la kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Tatu na Ligi Daraja la Nne.

Mwaka 1997 Ligi Kuu ikaanzishwa kama ligi ya juu zaidi na kuanza zama mpya, na hapo ndipo sasa kukawa na madaraja matano; Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Tatu na Ligi Daraja la Nne. Itakapofika mwaka 2027 Ligi Kuu itafikisha miaka 30.

MIAKA 03

Sasa kwa kuangalia kinachofayika kwenye Bongofleva, najiuliza kwa sauti, je wachezaji wa zamani wakiamua kutembea mikoani na kucheza mechi za hisani kuenzi miaka 30, watapata watu kama BongoFleva? Timu zikizokuwepo 1997 ni Yanga, Simba, Maji Maji, Mtibwa Sugar, Milambo

TZ Prisons, Tukuyu Stars, CDA, Kagera Stars, Pamba, Reli na Sigara.

Lakini, Lipuli FC ya Iringa na Coastal Union ya Tanga zilipanda daraja kushiriki Ligi Kuu mwaka 1998 kuchukua nafasi za Reli ya Morogoro na Sigara ya Dar es Salaam zilizoshuka. Tuzichukue timu hizi na wachezaji wake waliokuwepo mwaka ule wacheze mechi mikoani katika mtiririko uleule wa Bongofleva.

MIAKA 01

Katika timu 12 zikizokuwepo mwaka 1997, timu tano hazipo kabisa; CDA (Dodoma), Sigara (Dar es Salaam), Tukuyu Stars (Mbeya) na Milambo (Tabora). Timu moja ya Majimaji ya Songea bado ipo, lakini katika madaraja ya chini kabisa.

Baadhi ya wachezaji waliokuwepo upande wa Yanga ni Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Ediliby Lunyamila, Sekilojo Chambua, John Mwansansu, Kaunda Mwakitope, Kenneth Mkapa, Ildifonce Amlima, Bakary Malima na kadhalika. Kwa Simba kulikuwa na kina Mohamed Mwameja, Stephen Nemes, Mwanamtwa Kihwelo, George Masatu, Alfonce Modest, Mathias Mulumba, Juma Amir, Thomas Kipese, Akida Makunda na kadhalika.

Timu ya Majimaji ilikuwa na kina Doyi Moke, Omar Kapilima, Fortenatus Dello Tumba, Maalim Saleh “Romario”, Amri Said “Stam”, Kelvin Haule, Omar Hussein, Shaibu Kabwangwa, Ally Mopelo, Omar Bunju, Willy Martin “Gari Kubwa”, David Mjanja, John Alex Godfrey Kikumbizi, Steven “Garrincha” na kadhalika.

Mtibwa Sugar kulikuwa na Mecky Maxime, John Masamaki (mfungaji bora) Kamba Lufo, Abubakari Mkangwa, Geoffrey Magoli, Masumbuko Hassan, Salum Mayanga, Manyika Peter, Said Mhando, Ramadhani Ngubiagai, Christopher Gaga na kadhalika, huku Milambo ikiwa na kina Hassan Mbaruku, Said Mshamu, Victor Kilowoko, Omari Kitumba, Noah Kilimanjaro, Ramadhani Hamisi, Abdallah Sungura, Wilfred Kidao, Athumani Kairo, Hemed Matobango, Paschal Mayala, Ahmed Mwinyimkuu, Njilu Mensa na kadhalika.

Kwa Tanzania Prisons kulikuwa na John Joseph (JJ), Wolaf Mwamlima, Gerard Hillu, Munyu Kassim, Ivo Mapunda, Oswald Morris, Avinitishi Abdallah, Lameck Sichula, Dennis Edwin, James Nestory na wenzao. Je, miaka 30 ya LIGI KUU itabamba?