Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwisho wa enzi: Mahrez, Samatta, Mendy kuikosa AFCON

ENZI Pict

Muktasari:

  • Wachezaji hao wanatoka Tanzania, Algeria, Ivory Coast, Senegal, Ghana na Tunisia, huku Mbwana Samatta na  Riyad Mahrez akiwa wa kwanza kutangaza uamuzi huo, kabla ya Seko Fofana kuwa wa mwisho Septemba 14.

WAKATI harakati za kusaka kufuzu kwa fainali ya Mataifa ya Afrika (PAMOJA AFCON2027) zikitarajia kuanza wiki hii tayari nyota nane wa Afrika wameamua kustaafu soka la kimataifa.

Wachezaji hao wanatoka Tanzania, Algeria, Ivory Coast, Senegal, Ghana na Tunisia, huku Mbwana Samatta na  Riyad Mahrez akiwa wa kwanza kutangaza uamuzi huo, kabla ya Seko Fofana kuwa wa mwisho Septemba 14.

Samatta alitangaza kustaafu Julai 7, baada ya kuichezea Taifa Stars kwa miaka 15, akiongoza Tanzania kufuzu kwa AFCON mara tatu.

Mahrez alitangaza kustaafu Julai 3, siku chache baada ya Algeria kuondolewa na Uswisi kwa mabao 2-0 katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia 2026. Winga huyo wa Al Ahli, mwenye miaka 35, alimaliza safari yake ya kimataifa akiwa na mechi 119 na mabao 40.

Mahrez anaondoka akiwa na kumbukumbu ya kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 akiwa na Algeria, akifunga mabao matatu katika michuano hiyo, ikiwamo bao la ushindi dhidi ya Nigeria kwenye nusu fainali. Julai 16, kiungo wa Ivory Coast, Jean Michael Seri, naye alitangaza kustaafu baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 11. Seri alimaliza akiwa na mechi 66 na mabao manne, huku akishiriki AFCON mara tano.

ENZ 01

Mafanikio yake makubwa yalikuwa kutwaa AFCON 2023 iliyofanyika mwaka 2024 nchini Ivory Coast, ambapo pia alichaguliwa katika kikosi bora cha mashindano hayo.

Senegal ilipoteza wachezaji wawili, akiwamo mshambuliaji Pape Cherif Ndiaye, aliyetangaza kustaafu Agosti 30. Alikuwa ameitumikia Senegal kwa miaka miwili, akicheza mechi 19 na kufunga mabao manne.

Ndiaye alishiriki AFCON 2025 na Kombe la Dunia 2026, huku michuano hiyo ya AFCON ikiwa bado sehemu ya mchakato wa rufaa ya Senegal katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) baada ya uamuzi wa CAF kuhusu fainali dhidi ya Morocco.

Rani Khedira naye alichagua kuachana na Tunisia baada ya kipindi kifupi. Kiungo huyo wa Union Berlin alibadili uraia kisoka na kuanza kuichezea Tunisia mwaka 2026, baada ya FIFA kuidhinisha mabadiliko hayo Machi.

ENZ 02

Alimaliza akiwa na mechi sita pekee, tatu kati ya hizo zikiwa katika Kombe la Dunia 2026. Khedira alieleza kuwa ulikuwa wakati wa kuangalia mbele na kuwapa nafasi vijana kujenga kizazi kipya cha timu hiyo.

Ghana nayo ilipoteza mshambuliaji Inaki Williams, aliyetangaza kustaafu Septemba 11. Williams alimaliza akiwa na mechi 28 na mabao mawili baada ya kuamua kuichezea Ghana mwaka 2022, licha ya awali kucheza mechi moja ya kirafiki kwa Hispania.

Alishiriki Kombe la Dunia 2022 na 2026 pamoja na AFCON 2023, huku mashindano ya mwaka huu yakiwa ya mwisho kwake akiwa na Black Stars.

Septemba 13, kipa wa Senegal, Edouard Mendy, alitangaza pia kustaafu baada ya miaka minane na timu hiyo. Mendy alicheza mechi 59 na kurekodi clinshiti 31, huku mafanikio yake makubwa yakiwa kutwaa AFCON 2021 na kutajwa kuwa kipa bora wa mashindano hayo.

ENZ 03

Mendy pia alishinda tuzo ya Kipa Bora FIFA mwaka 2022 na kushiriki Kombe la Dunia la 2022 na 2026.

Mchezaji wa mwisho kutangaza uamuzi huo ni Seko Fofana wa Ivory Coast, aliyestaafu Septemba 14 akiwa na miaka 31. Fofana alicheza mechi 34 na kufunga mabao saba kwa Tembo hao.

Alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa AFCON 2023 na pia alishiriki Kombe la Dunia 2026, kabla ya Ivory Coast kuondolewa na Norway katika hatua ya 32 bora.

Kwa ujumla, Ivory Coast na Senegal zimeathirika zaidi kwa kupoteza wachezaji wawili kila moja, huku Tanzania, Algeria, Ghana na Tunisia zikipoteza mchezaji mmoja mmoja.