Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Njia ngumu kwa Arsenal, Liverpool, Man City Ligi ya Mabingwa

NJIA Pict

Muktasari:

  • Timu hizo ndizo zitakazowakilisha England katika msimu huu wa mashindano hayo, huku mashabiki wakishuhudia mfumo mpya wa michuano hiyo ukiendelea kutumika.

LONDON, ENGLAND: MIAMBA ya England klabu za Arsenal, Aston Villa, Liverpool, Manchester City na Manchester United ratiba ya mechi zao katika hatua ya ligi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu imetoka, huku baadhi zikikabiliwa na mechi ngumu mwanzoni mwa kampeni zao.

Timu hizo ndizo zitakazowakilisha England katika msimu huu wa mashindano hayo, huku mashabiki wakishuhudia mfumo mpya wa michuano hiyo ukiendelea kutumika.

Baada ya kuwajua wapinzani wao Alhamisi, UEFA sasa imetangaza tarehe na muda wa michezo yote ya hatua hiyo.

Aston Villa itaanza kampeni yake dhidi ya Club Brugge Jumanne, Septemba 8, saa 5:45 usiku, kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza nyumbani dhidi ya Fenerbahce Jumatano, Oktoba 14, saa 8:00 usiku.

Villa itakuwa na michezo miwili mfululizo nyumbani ikimaliza dhidi ya Viking FK Jumanne, Oktoba 21, saa 8:00 usiku. Baada ya hapo itasafiri kwenda Nou Camp kuikabili Barcelona Jumanne, Novemba 3, saa 8:00 usiku, kabla ya kucheza na Galatasaray Jumanne, Novemba 24, saa 5:45 usiku.

NJI 01

PSG itafika Villa Park Jumanne, Desemba 8, saa 8:00 usiku, huku Borussia Dortmund ikiwa mpinzani wao wa mwisho nyumbani Jumanne, Januari 19.

Villa itafunga kampeni yake kwa kusafiri kwenda Jamhuri Czech kucheza na Slavia Prague Jumatano, Januari 27, saa 8:00 usiku.

Mabingwa Arsenal, ambayo ilipoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, itakutana na Napoli katika mchezo wake wa kwanza Jumatano, Septemba 9, saa 8:00 usiku.

Baada ya hapo itamkaribisha Lille katika Uwanja wa Emirates, kabla ya kusafiri kwenda Ujerumani kuikabili Bayern Munich katika Uwanja wa Allianz Arena Jumatano, Oktoba 21, saa 8:00 usiku.

Mchezo unaofuata wa Arsenal utakuwa ugenini dhidi ya Slavia Prague Jumatano, Novemba 4, saa 8:00 usiku.

Borussia Dortmund na Real Madrid ni miongoni mwa wapinzani watakaokutana na Arsenal katika mechi zinazofuata, huku timu hiyo ya Mikel Arteta ikiwa mwenyeji wa michezo hizo Emirates.

NJI 02

Arsenal pia itasafiri kwenda Hispania kuikabili Real Betis katika Uwanja wa Benito Villamarin kabla ya kumaliza hatua hiyo nyumbani dhidi ya Sabah FC.

Liverpool nayo itaanza kampeni yake kwa mchezo mkubwa dhidi ya Atletico Madrid Jumatano, Septemba 9, saa 8:00 usiku, kwenye Uwanja wa Anfield.

Baada ya hapo itasafiri kucheza na LASK Jumatano, Oktoba 14, saa 5:45 usiku, kabla ya kuikaribisha Villarreal Jumanne, Oktoba 20, saa 8:00 usiku.

Liverpool itakwenda Istanbul kuikabili Fenerbahce Jumatano, Novemba 4, saa 5:45 usiku, kabla ya kusafiri kwenda Ubelgiji kucheza na Club Brugge wiki tatu baadaye.

Porto itafika Anfield Jumatano, Desemba 9, saa 8:00 usiku, huku Liverpool ikisafiri kwenda Italia kucheza na Inter Milan katika Uwanja wa San Siro Jumanne, Januari 19.

Mchezo wao wa mwisho utakuwa nyumbani dhidi ya Lens Jumatano, Januari 27, saa 8:00 usiku. Manchester City itafungua kampeni yake kwa kusafiri kwenda Lisbon, Ureno, kucheza na Porto Jumanne, Septemba 8, saa 8:00 usiku.

NJI 03

Mchezo wa pili utakuwa nyumbani dhidi ya PSG Jumatano, Oktoba 14, saa 8:00 usiku, kabla ya kuikaribisha AEK Athens Jumanne, Oktoba 20.

City itasafiri kwenda Ujerumani kucheza na RB Leipzig Jumatano, Novemba 4, kabla ya kukutana na Napoli Jumanne, Novemba 24. Barcelona itakuwa mpinzani wao unaofuata katika Uwanja wa Nou Camp Jumanne, Desemba 8, saa 8:00 usiku.

City itacheza na Lens ugenini Jumatano, Januari 20, kabla ya kumaliza hatua hiyo kwa kuikaribisha Sporting Lisbon katika Uwanja wa Etihad Jumatano, Januari 27.

Kwa upande wa Manchester United, kocha Michael Carrick ataanza safari yake ya kwanza ya Ulaya akiwa na mamlaka kamili ya kuiongoza timu hiyo kwa kuikaribisha Sabah FC katika Uwanja wa Old Trafford Alhamisi, Septemba 10, saa 8:00 usiku. United itasafiri kwenda Madrid kuikabili Atletico Madrid Jumanne, Oktoba 13, saa 8:00 usiku, kabla ya kwenda Italia kucheza na Como Jumatano, Oktoba 21, saa 5:45 usiku. Roma itafika Old Trafford Jumanne, Novemba 3, saa 8:00 usiku, huku United ikisafiri kwenda Lisbon kuikabili Sporting Jumatano, Novemba 25.

Baadaye United itamkaribisha RB Leipzig Old Trafford Jumanne, Desemba 8, saa 8:00 usiku, kabla ya kwenda kucheza na Bayern Munich Jumatano, Januari 20. Mechi ya mwisho ya United itakuwa dhidi ya Villarreal nchini Hispania Jumatano, Januari 27, saa 8:00 usiku.

Mechi zote 18 za raundi ya mwisho ya hatua ya ligi zitachezwa kwa wakati mmoja Januari 27, hatua ambayo inalenga kuhakikisha hakuna timu inayopata faida kwa kujua matokeo ya wapinzani wake kabla ya kucheza.

Miongoni mwa michezo hiyo ni Shakhtar Donetsk kuikaribisha Real Madrid katika Uwanja wa Stamford Bridge, ambao klabu hiyo ya Ukraine inautumia kama uwanja wake wa muda.