Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sarakasi za Ballon d'Or mwaka huu

PUMZI Pict


Kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 69 ya tuzo za Ballon d'Or, waandaaji wake wamejitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi kuhusu uhusiano wa tuzo hizo na Kombe la Dunia.


Katika tovuti rasmi ya Ballon d'Or, waandaaji hao ambao ni jarida la France Football, wamewaandaa kisaikolojia wafuatiliaji wa tuzo hizo kabla mshindi hajatangazwa.


Katika taarifa yao iliyochapishwa Julai 20, Ballon d'Or wameweka wazi kushinda Kombe la Dunia hakutengenezi uhakika wa kushinda tuzo hiyo. Hii ina maana kuna uwezekano mkubwa sana mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu akatoka nje ya Kombe la dunia.

PUMZ 01

Hiki siyo kitu kigeni kwa sababu tangu mwaka 1955 tuzo hizo zilipoanza, zimeshatolewa mara 69 kwa wachezaji 39 tofauti na kati ya hao ni wachezaji saba tu ambao walishinda Ballon d'Or kwa sababu ya kushinda Kombe la Dunia.


Bobby Charlton           (England 1966)

Paolo Rossi     (Italia 1982)

Lothar Matthäus         (Ujerumani Magharibi 1990)

Zinedine Zidane           (Ufaransa 1998)  

Ronaldo de Lima         (Brazil 2002) 

Fabio Cannavaro         (Italia 2006)

Lionel Messi    (Argentina 2022)


Kwa hiyo hakuna ajabu kwa walichokisema, lakini kwa nini waseme...na kwa nini sasa? Miaka yote ya Kombe la Dunia Ballon hutoka na hawatoi ufafanuzi wa jambo lolote...wanataka kufanya nini safari hii?

PUMZ 06

Hivi ni nani ambaye hajui kushinda Kombe la Dunia sio tiketi ya kushinda Ballon d'Or? Watu wote walikuwa wanajua hivyo, hadi wao wenyewe walivyoanza kuyabananga na kuyabagaza mambo.

Kila kitu kilikuwa kinaenda sawa na mchezaji aliyefanya vizuri kuliko wote ndani ya mwaka husika alipewa tuzo hiyo. Lakini kuanzia mwaka 2010 mambo yalibadilika kutokana na wao wenyewe kubadilisha vigezo bila maelezo yoyote.

PUMZ 05

2010 YALIANGALIWA MABAO YA MESSI

Wesley Sneijder wa Uholanzi aliiongoza klabu yake ya Inter Milan ya Italia kushinda mataji matatu yaani treble ambayo ni Ligi ya Mabingwa Ulaya, Serie A na Copa di Italia.

Huo pia ulikuwa mwaka wa kombe la Dunia na Wesley Schneider akaiongoza timu yake ya taifa, Uholanzi, kufika fainali huku akiwa mfungaji bora wa mashindano. Uholanzi ilipoteza fainali kwa Hispania ambayo nyota wake Andreas Iniesta aling'ara kweli kweli, akifunga bao la ushindi.

Kwenye Kombe la Dunia, Messi hakufunga hata bao moja, aliishia kutoa pasi moja tu ya bao...tena ya offside, kwa Carlos Tevez dhidi ya Mexico hatua ya 16 bora. Timu yake ikatolewa robo fainali kwa kichapo cha 4-0 kutoka kwa Ujerumani. Messi na Iniesta walikuwa klabu moja, Barcelona na walishinda La Liga pamoja.

Zilipokuja tuzo za Ballon d'Or Messi akatangazwa mshindi, eti kwa sababu alifunga mabao mengi ndani ya huo mwaka. Alifunga mabao 60 akatoa pasi 17 katika mechi 64. Hayakuangaliwa makombe aliyoshinda Wesley Schneider na mchango wake kwenye hayo makombe. Hayakuangaliwa mabao yake yaliyoipeleka Uholanzi fainali ya Kombe la Dunia. Hayakuangaliwa makombe ya Iniesta na mchango wake kwa Hispania kushinda Kombe la Dunia. Haukuangaliwa mchango wake kwa Barcelona kushinda La Liga.

Yakaangaliwa tu mabao ya Messi na pasi zake za magoli...akashinda Ballon d'Or.

PUMZ 04

2011 VILIANGALIWA VIKOMBE VYA MESSI

Cristiano Ronaldo alifunga mabao mengi kuliko Messi, lakini safari hii makombe yakawa vigezo, sio mabao na alifunga mabao 60 na pasi 18 za mabao kwenye mechi 54 za mwaka husika.

Messi akiwa na Barcelona alifunga mabao 59 na kushinda La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

PUMZ 03

2012 YALIANGALIWA MABAO YA MESSI

Mwaka 2012 Messi alifunga mabao 91 ndani ya mwaka huo, lakini Ronaldo alishinda mataji mengi.

Messi akiwa na Barcelona hawakushinda taji lolote, lakini Ronaldo akiwa na Real Madrid alishinda La Liga na Supercopa Espana.

Lakini, mataji ya Ronaldo hayakuangaliwa, bali yakaangaliwa mabao ya Messi.

PUMZ 02

2019 YALIANGALIWA MABAO YA MESSI

Mo Salah, Virgil van Dijk na Alisson Bekker wa Liverpool walikuwa na msimu bora sana wakishinda mataji makubwa ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Zaidi ya hapo Alisson Bekker akashinda na Copa America.

Kwa kigezo cha mataji, hawa walikuwa na mataji mengi na ndio walikuwa vinara wa timu yao.

Messi na Barcelona yake walishinda La Liga tu na kwenye ligi ya mabingwa walitolewa nusu fainali na Liverpool ya hawa jamaa watatu.

Lakini tuzo zikayaangalia mabao ya Messi, sio mataji ya kina Salah na VVD au Alisson Bekker.


2021 YALIANGALIWA MATAJI YA MESSI

Mwaka huu Roberto Lewandowski wa Bayern Munich alifunga mabao mengi kuliko Messi na alifunga mabao 69 huku Messi akifunga 41.

Lakini, Messi akashinda Ballon d'Or kwa sababu akiwa na Argentina walitwaa Copa America...vigezo vikawa vimebadilika tena.

PUMZ 07
PUMZ 07

2023 YALIANGALIWA MATAJI YA MESSI

Messi ambaye hadi hapa alikuwa anacheza soka Marekani, aliiongoza Argentina kushinda Kombe la Dunia Desemba 2022.

Mwaka 2010 Kombe la Dunia halikuwa na maana kwenye Ballon d'Or, lakini safari hii lilipewa uzito. Zaidi ya Kombe la Dunia Messi hakushinda kitu chochote kwenye klabu yake au yeye mwenyewe. Lakini akachukua Ballon d'Or.

Na waandaaji wa tuzo hawakuwahi kutoa ufafanuzi wowote kuhusu chochote kilichotokea. Safari hii, mwaka 2026 wanakuja hadharani na kusema Kombe la Dunia siyo tiketi ya moja kwa moja kushinda Ballon d'Or, kwani 2023 ilikuwaje? Ndiyo maana tunasema Ballon d'Or ni kigeugeu.