Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kurudia ilichofanya 2009/10 CAFCL?

Muktasari:

  • Timu hiyo imekuwa na mwenendo mzuri msimu huu ikiwa ndiyo pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa katika Ligi Kuu Bara na ya Ligi ya Mabingwa Afrika imetinga makundi kama zilivyo zingine tatu kutoka Bara.

MASTAA wa zamani wa Simba wamezungumzia mwenendo wa timu hiyo wakiamini rekodi iliyowekwa msimu wa 2009/10 inaweza kujirudia huu, endapo wachezaji wataamua kukaza hadi mwisho.

Timu hiyo imekuwa na mwenendo mzuri msimu huu ikiwa ndiyo pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa katika Ligi Kuu Bara na ya Ligi ya Mabingwa Afrika imetinga makundi kama zilivyo zingine tatu kutoka Bara.

Msimu wa 2009/10, timu zilizokuwa zikishiriki Ligi Kuu Bara zilikuwa 12. Katika mechi 10, Simba ilishinda zote ikifanikiwa kufunga mabao 19 na kufungwa matatu. Tofauti na msimu huu wa 2026/27, ambapo timu zipo 16, timu hiyo katika mechi 10 haijapoteza, ikikusanya mabao 23 na kufungwa sita.

Msimu wa 2009/10, Simba ilichukua ubingwa ikiwa na pointi 62 katika mechi 22, ikishinda 20 na kutoka sare mbili, bila kufungwa mechi hata moja.

Mwanaspoti limezungumza na mastaa mbalimbali wa timu hiyo wanaoamini Simba imerejea kwenye kiwango bora na kuna uwezekano mkubwa wa kurudia rekodi ya 2009/10 ya kuchukua ubingwa bila kufungwa, lakini mastaa wanapaswa kujua wana kazi kubwa ya kufanya.

Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi ambaye msimu wa 2009/10 ndiye alikuwa kinara wa mabao 18 Ligi Kuu Bara, alisema mafanikio yao yalitokana na kuambiana ukweli na kila mchezaji kuchukulia malengo ya timu kuwa kipaumbele. Ushin dani wa namba ulikuwa mkubwa, jambo lililowasaidia kujituma kwa bidii.

“Wachezaji tulikuwa na vikao vyetu, kwa wiki tulikuwa tunakaa mara mbili ili kujadiliana kile tulichokifanya uwanjani. Mwenzetu akikosea tunamwambia hapa ulikuwa na uwezo mkubwa wa kuibeba timu, imekuaje ukacheza kiwango cha chini,”  alisema Mgosi na kuon geza:

“Tulikuwa na upendo, umoja, hakuna mchezaji aliyekuwa akitanguliza maslahi yake. Tulifanya kwa ajili ya timu kuhakikisha mashabiki wanapata raha, ndiyo maana tulichukua ubingwa bila kufungwa.”

Alisema wachezaji wa Simba waliopo wana uwezo mkubwa, lakini watambue ligi si nyepesi na kunahitajika mapambano hadi mwisho.

“Ukiangalia kiwango cha ushindani kipo sawa, hata zikikutana timu za madaraja ya kati zinakuwa na ushindani mkali. Kikubwa, mastaa wa Simba wajue wana kazi ya kuwapa kicheko mashabiki wao,” alisema mkongwe huyo.

Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo na Taifa Stars, Danny Mrwanda, alisema: “Kilichotubeba tulikuwa wakweli. Ukiona mchezaji mwenzako alikuwa na uwezo wa kufanya kitu hajafanya, anaambiwa ukweli kwa upendo. Lakini pia viongozi walikuwa bega kwa bega na timu, wanakuja mazoezini, kambini, hivyo tulipata hamasa kubwa. Naamini hilo linaweza likajirudia msimu huu endapo wakiamua kukaza buti.”

Aliyekuwa mwenyekiti wa Simba kipindi hicho, Hassan Dalali Field Marshal alisema: “Jambo la kwanza ambalo lilitusaidia nyakati hizo kuweka rekodi ya kutofungwa hadi kuchukua ubingwa, kwanza niliishi maisha ya wachezaji, sikutengeneza madaraja. Kuna wakati nilikunywa maji ya madumu kama wao, nililala kambini muda mwingine kama wao. Niliwapa moyo wa upambanaji. Ninachokiona msimu huu inaweza ikajirudia rekodi hiyo endapo wachezaji wakiamua kupambana hadi tone la mwisho,” alisema Dalali.

“Mfano mzuri ni kile walichofanya dhidi ya Namungo FC. Aliongeza: Endapo Simba ikichukua ubingwa bila kufungwa, jambo la kwanza, tamasha la mwaka huu lilifanyika Uhuru na kwa mara ya kwanza lilifanyikia uwanja huo huo, na msimu wa 2009/10 ulikuwa uwanja wetu wa nyumbani.”