Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukurasa mwingine wa Yao Yanga

Muktasari:

  • Ndio ni kweli kinachofanya mashabiki wazungumze hilo ni kutokana na kiwango bora alichoendelea kukionyesha kwenye klabu hiyo licha ya kutoka kwenye kipindi kigumu cha majeraha.

KUNA wachezaji huvaa jezi ya Yanga, lakini Yao Attohoula anaonekana kuivaa na kuimiliki. Namna anavyopambana, anavyokimbia, anavyokaba na kujituma upande wa kulia imeanza kuwafanya mashabiki kusema beki huyo anacheza kana kwamba ni mwanachama wa klabu.

Ndio ni kweli kinachofanya mashabiki wazungumze hilo ni kutokana na kiwango bora alichoendelea kukionyesha kwenye klabu hiyo licha ya kutoka kwenye kipindi kigumu cha majeraha.

Namna beki huyo wa kulia alivyoanza msimu mpya akiwa na dalili za kurudisha kiwango chake cha zamani.

Baada ya kupitia kipindi ambacho majeraha yalimfanya akae nje ya uwanja kwa muda mrefu, amerejea akiwa na utulivu, kasi na ujasiri uleule uliomfanya kuwa chaguo la kwanza Yanga.

KUTOKA KWENYE MAJERAHA

Yao alijiunga na Yanga Julai 2023 na ndani ya muda mfupi akaonyesha kwa nini alipewa nafasi katika kikosi hicho. Kasi, nguvu, uwezo wa kupanda kusaidia mashambulizi na kurudi kwa haraka kwenye ulinzi vilimfanya kuwa mmoja wa mabeki waliokuwa na umuhimu mkubwa kwenye mfumo wa Yanga.

Alicheza msimu mmoja na nusu na Januari 2025, alipata jeraha la goti la kushoto, lililohitaji upasuaji na kumuweka nje kwa muda mrefu.

Baada ya kupona jeraha hilo ilidaiwa alijitonesha tena mazoezi hivyo ikamfanya akae muda mrefu hadi alipofanyiwa upasuaji.

Katika kipindi hicho nafasi yake ilizibwa na Israel Mwenda ambaye alisajiliwa dirisha dogo akitokea Singida Black Stars alionyesha uwezo mkubwa kila alipopata nafasi.

MUUNGANO UKAWA MWANZO

Baadhi ya mashabiki waliamini majeraha ya beki huyo yangemuweka nje muda mrefu na hakukuwa na changamoto kwenye nafasi yake kutokana na Mwenda kuonyesha kiwango bora.

Lakini baada ya kurejea alianza kupewa mechi za mashindano ya Muungano yakamsaidia kumrejesha kwenye kiwango chake.

Tofauti na mechi za ushindani mkubwa wa ligi au michuano ya kimataifa, mashindano hayo yalimpa nafasi ya kucheza bila presha kubwa. Alianza taratibu, akionekana bado kujitafuta, lakini kila mechi aliyocheza ilionyesha dalili za kurejea kwa ubora wake.

Kilichoonekana wazi zaidi ni kujiamini kwake. Yao alianza tena kufanya vile vitu ambavyo vilimfanya awe miongoni mwa mabeki bora wa kulia nchini. Alikuwa mkali kwenye mipira ya kugombea, mwenye uthubutu wa kupanda mbele na mwenye usomaji mzuri wa mchezo.

Mechi aliyokuwa na kiwango bora na kuwaibua mashabiki ni ile ya fainali dhidi ya watani zao Simba, Yao alicheza dakika 45 akikaba na kushambulia kwa usahihi.

Mwisho wa msimu uliopita ulikuwa muhimu zaidi kwa sababu Yao hakumaliza tu mashindano akiwa amerejea uwanjani, bali alianza kuonyesha kiwango ambacho kilifanya ushindani wa nafasi ya beki wa kulia kuwa mkubwa zaidi.

Katika mechi dhidi ya Simba, aliingia kipindi cha pili na kuleta uhai upande wa kulia. Baadaye akapewa dakika 62 dhidi ya KMC na kuonyesha mwendelezo mzuri.

FAIDA KWA YANGA

Faida kubwa kwa Yanga ni kwamba anaiunganisha safu ya ulinzi na mashambulizi bila kuifanya timu ipoteze uwiano. Beki huyo anapanda kushambulia, anapanua uwanja na kumfungulia nafasi winga au kiungo mshambuliaji kuingia ndani. Hilo linaendana na namna Yanga inavyotumia mabeki wa pembeni kama njia ya kuendeleza mashambulizi.

Lakini kinachomtofautisha zaidi Yao ni uwezo wa kufika haraka kwenye matukio. Anapopanda na timu ikapoteza mpira, kasi yake inampa nafasi ya kurejea mapema na kusaidia kuziba upande wake.

Hivyo Yanga inaweza kupata faida ya kuwa na mchezaji anayesaidia kutengeneza mashambulizi bila kulazimisha timu kubaki wazi upande wa kulia.

Kwenye mechi za kimataifa hususani za Ligi ya Mabingwa ambazo hukutana timu mbalimbali bora Yao anaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine.

HISTORIA INAONYESHA

Mbali na Yao baadhi ya nyota waliowahi kupata majeraha kwenye ligi yaliyowaweka muda mrefu lakini walirejea wakiwa na kiwango bora.

Miongoni mwao ni nahodha wa Simba, Shomari Kapombe ambaye mwaka 2020 alipata jeraha la goti lililomuweka nje kwa takribani msimu mzima lakini baada ya kurejea aliendelea kuwa sehemu muhimu ya timu.

Aishi Manula naye kabla ya kujiunga na Azam FC msimu wa 2025/25 akiwa Simba alipata jeraha la bega lililomfanya akae muda mrefu lakini alipotimkia mitaa ya Chamazi alikuwa na kiwango bora msimu uliopita,

Kama ataendelea na kiwango alichoanza kukionyesha baada ya kurejea, Yanga itakuwa imepata zaidi ya beki wa kulia. Itakuwa imepata mchezaji anayejua majukumu yake, anayejua presha ya klabu na ambaye tayari ameshapitia vita ya kurejea kutoka kwenye jeraha kubwa.