Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bactash aandika rekodi Ligi Kuu Zanzibar

BACTASH Pict

Muktasari:

  • Bactash alifunga mabao matatu katika ushindi wa 4-1 ilioupata Muembe Makumbi City dhidi ya Kipanga, mchezo uliochezwa Oktoba 2, 2026 kwenye Uwanja wa Mao B, Unguja.

MSHAMBULIAJI wa Muembe Makumbi City, Bactash Ali Bakari, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Bactash alifunga mabao matatu katika ushindi wa 4-1 ilioupata Muembe Makumbi City dhidi ya Kipanga, mchezo uliochezwa Oktoba 2, 2026 kwenye Uwanja wa Mao B, Unguja.

Mshambuliaji huyo alifungua akaunti mapema dakika ya pili kabla Ibrahim Samuel hajaongeza la pili dakika ya 42. Fredrick Godwin aliifungia Kipanga bao la kufutia machozi dakika ya 44, kabla Bactash kukamilisha hat-trick yake kwa mabao mawili dakika ya 60 na 83.

Mabao hayo yamemfanya Bactash kuingia kwenye orodha ya vinara wa ufungaji akiwa na manne, akilingana na mshambuliaji wa Zimamoto, Rashid Salim Salum.

Bactash si mgeni wa kufunga mabao, kwani msimu wa 2025-26 akiwa KMKM alihusika na mabao 13, huku akifunga 10 na kutoa asisti tatu.