Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker amuandaa kisaikolojia mido

BARKER Pict


SIMBA jana ilikuwa uwanjani ikicheza dhidi ya Geita Gold, lakini siku moja kabla ya mchezo huo, kocha wa kikosi hicho, Steve Barker alikaa na kiungo, Ibraheem Jabaar akimuandaa kisaikolojia wakati akielekea kumaliza adhabu yake.


Jabaar amekuwa nje kwa mechi tatu akitumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji, baada ya kunaswa na Teknolojia ya Football Video Support System (FVS) akimpiga kiwiko mchezaji wa wapinzani.


Baada ya kadi hiyo, Jabaar alikuwa nje na mechi dhidi ya Geita Gold, kiungo huyo ndio amemaliza adhabu yake ya kukosa michezo mitatu na sasa atarejea uwanjani kuanzia mechi ijao dhidi ya Azam itakayopigwa Septemba 9, 2026.

BARK 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Barker amesema amefanya mazungumzo na kiungo huyo na amemweleza anavyotakiwa kubadilika kutokana na matukio ambayo yanaweza kufanyika kwa kificho na kuonekana kwa marudio ya video.

“Jabaar anamalizia adhabu yake, wakati wowote tutakuwa naye lakini kitu cha msingi ameimarika kiakili kutokana na kilichotokea, alijua amekosea, namjua ni mtu ambaye hana rekodi ya kuwa na matukio ya utukutu,” amesema Barker ambaye aliwahi kufanya kazi na Mnigeria huyo wakiwa Stellenbosch ya Afrika Kusini.

“Nimemwambia anavyotakiwa kutambua kuna wakati kwa jina lake na ukubwa wa klabu anayoitumikia, anaweza kuchokozwa ili afanye makosa kama yale na akijibu anaweza kuingia katika mtego, hivyo hatakiwi kufanya tena na amenielewa.”

BARK 02

Barker ameongeza, siyo tu kwa Jabaar, amekuwa akiwakumbusha wachezaji wake kila wanapotaka kuingia uwanjani kuwa makini na matukio ya kucheza vibaya na hataki kuona wanakutana tena na mazingira ya kupata kadi nyekundu.

“Hatuhitaji tena kuwa na matukio ya namna hii, yanatuumiza makocha, pia mashabiki, tumekuwa tukiwakumbusha wachezaji namna ya kucheza kwa umakini hasa wakati kama huu ambao kuna nafasi ya mwamuzi kurudi nyuma na kuangalia matukio yaliyopita.”

BARK 03

Simba katika mechi nne zilizopita kabla ya kucheza na Geita Gold, wachezaji wake watatu wameshakumbana na adhabu ya kadi nyekundu wakiwemo mabeki David Kameta ‘Duchu’, Jabaar na Antony Mligo.

Kadi hizo tatu zimeweka rekodi kubwa na mbaya kwa Simba ikiwa ndiyo timu iliypata kadi tatu mfululizo, pia ikiwa timu ambayo imezalisha kadi nyingi nyekundu hadi sasa na zote zikipatikana baada ya marudio ya usaidizi wa video kwa waamuzi.