Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beimbaya achimba mkwara Championship

BEIMBAYA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi nane za Kigamboni United hadi sasa, imeshinda tatu, sare tatu na kupoteza mbili, ikishika nafasi ya nane na pointi 12, huku safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho ikifunga mabao tisa na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara saba.

KOCHA Mkuu wa Kigamboni United zamani B19 FC, Twaha Beimbaya amesema malengo ya timu hiyo kwa sasa ni kupigania nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2027-2028, jambo ambalo linawezekana licha ya ushindani mkubwa unaoendelea sasa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Beimbaya amesema jambo linalompa matumaini ni kutokana na kutopishana pointi nyingi zaidi na washindani wao, huku akijivunia mradi mzuri wa wachezaji bora wa timu hiyo wanaoendelea kuonyesha kiwango cha kuvutia.

"Mwenendo wetu sio mbaya kutokana na pointi tulizonazo hadi sasa, nadhani baada ya kumaliza raundi 15, za kwanza, ndipo nitakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kutathimini, japo hapa tulipo ni pazuri na tunapaswa kupashikilia," amesema Beimbaya.

Kocha huyo aliyeifundisha Kiluvya United kwa sasa Barberian FC na Pan Africans, amesema ahadi yake ya kutengeneza kikosi cha ushindani inaendelea kutimia taratibu, licha ya ushindani na ugumu wa Ligi ya Championship tangu msimu huu umeanza.

Katika mechi nane za Kigamboni United hadi sasa, imeshinda tatu, sare tatu na kupoteza mbili, ikishika nafasi ya nane na pointi 12, huku safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho ikifunga mabao tisa na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara saba.