Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bwamkuu: Mashujaa Queens sasa kazi ipo Moshi

BWAMKUU Pict

Muktasari:

  • Neema Paul alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Fountain Gate katika mchezo wa msimu uliopita dhidi ya Mashujaa, kabla ya kuhamia kwa wapinzani hao, jambo linaloongeza ladha katika ushindani wa timu hizo.

KOCHA wa Mashujaa Queens, Rajab Ally 'Bwamkuu' amesema ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fountain Gate Princess katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (WPL) msimu wa 2026/27 ni mwanzo mzuri wa safari yao, lakini amesisitiza kikosi hicho kinapaswa kujiandaa kwa mtihani mwingine dhidi ya Kilimanjaro Wonders utakaochezwa Novemba 4, mwaka huu.

Mashujaa ilipata ushindi huo ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Oktoba 28, 2026.

Akizungumza na Mwanaspoti Bwamkuu amesema haikuwa mechi rahisi licha ya timu yake kuondoka na pointi tatu, akieleza matokeo hayo pamoja na malengo waliyoweka kabla ya msimu kuanza yanawapa dira nzuri ya kuendelea kupambana katika mashindano hayo.

“Kweli tumepata ushindi ugenini dhidi ya Fountain Gate lakini haikuwa rahisi. Malengo tuliyoyaweka kwa msimu huu na matokeo tuliyoyapata katika mchezo wetu wa kwanza yanatupa dira na uelekeo mzuri kwa msimu wa 2026/2027,” amesema kocha huyo.

Hata hivyo, Bwamkuu ameelekeza nguvu zake kwenye mchezo ujao dhidi ya Kilimanjaro Wonders, utakaopigwa mjini Moshi, akitambua wapinzani hao watakuwa na kiu ya kurekebisha makosa baada ya kuanza msimu kwa kupoteza mabao 3-0 dhidi ya Simba Queens kwenye Uwanja wa Ushirika.

“Tunaamini hautakuwa mchezo rahisi, kwani wametoka kupoteza dhidi ya Simba,” amesema Bwamkuu na maandalizi ya kikosi chake yanapaswa kuendelea kwa umakini.

Ushindi huo wa Mashujaa una umuhimu wa kipekee ukizingatia historia ya timu hizo msimu uliopita na kila moja iliichapa mwenzake.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Babati, Fountain Gate iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Rehema Mohamed, lakini Mashujaa ikalipa kisasi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo wa marudiano uliochezwa nyumbani.

Mbali na maandalizi na ubora wa kikosi, usajili wa wachezaji waliokuwa Fountain Gate Princess, Neema Paul na Neema Charles, ambao sasa wanaitumikia Mashujaa Queens, ni sehemu ya mabadiliko yaliyoongeza nguvu katika kikosi hicho.

Neema Paul alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Fountain Gate katika mchezo wa msimu uliopita dhidi ya Mashujaa, kabla ya kuhamia kwa wapinzani hao, jambo linaloongeza ladha katika ushindani wa timu hizo.