Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania atamani haya Uturuki

NASMA Pict

Muktasari:

  • Manduta, ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Antalya Spor baada ya kuondoka Ceasiaa Queens ya Iringa, kabla ya hapo aliwahi kuzitumikia Yanga Princess, Baobab Queens na Get Program. Pia aliwahi kuitwa katika kikosi cha Taifa kilichoshiriki Kombe la Dunia la Futsal la Wanawake mwaka 2025, Philippines.

Kiungo mshambuliaji wa Tanzania, Nasma Manduta anayekipiga 1207 Antalya Spor Kulübü amesema kucheza ligi ya Uturuki ni mwanzo wa safari yake ya kutafuta kucheza ligi kubwa Ulaya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Manduta amesema hadi sasa ameshacheza mechi tano akiwa na timu hiyo, mbili za kirafiki na tatu za ligi na amekutana na ushindani mkubwa unaompa changamoto ya kujifunza na kujiongeza zaidi ili kuendana na mazingira ya soka la nchini humo.

"Kiukweli ni ligi ngumu na yenye ushindani mkubwa sana. Hadi sasa nimecheza mechi tano mbili za kirafiki na mbili za ligi, hivyo ninaendelea kujifunza na kuzoea mazingira ya hapa," amesema Manduta.

NAS 01

Ameongeza kwa sasa anachezeshwa nafasi ya kiungo mkabaji, namba sita, ambayo inahitaji umakini mkubwa katika kukaba, kuzuia mashambulizi na kuanzisha mashambulizi ya timu.

Hata hivyo, ameeleza si mara yake ya kwanza kucheza nafasi hiyo, hivyo anachokipa kipaumbele ni kuongeza mazoezi binafsi ili kuimarika zaidi.

"Kwa sasa nachezeshwa kiungo namba sita. Ni nafasi ngumu, ingawa si mara yangu ya kwanza kucheza hapo. Kikubwa ninachopaswa kufanya ni kuongeza mazoezi ya ziada ili nizidi kujiimarisha katika eneo hilo," amesema.

NAS 02

"Ninazidi kumwomba Mungu kila siku aniongoze na kiwango changu kizidi kuwa bora. Natamani hapa pawe mwanzo wa safari nyingine katika maisha yangu ya soka, niendelee kupeperusha vizuri bendera ya nchi yangu na kulitangaza jina langu," amesema.

Manduta, ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Antalya Spor baada ya kuondoka Ceasiaa Queens ya Iringa, kabla ya hapo aliwahi kuzitumikia Yanga Princess, Baobab Queens na Get Program. Pia aliwahi kuitwa katika kikosi cha Taifa kilichoshiriki Kombe la Dunia la Futsal la Wanawake mwaka 2025, Philippines.