Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Clara Luvanga na kibarua kingine Saudia

CLARA Pict

Muktasari:

  • Macho ya Watanzania yatakuwa kwenye mchezo huo kushuhudia wabongo wanaokipiga kwenye ligi hiyo nini watakachokifanya baada ya kuwa na muendelezo mzuri kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Asia.

KESHO Septemba Mosi, Al Nassr Women itakuwa na kibarua kingine safari hii katika nusu fainali ya Kombe la Super Cup dhidi ya Al Ahli mchezo utakaopigwa Uwanja wa King Fahd Sport City.

Macho ya Watanzania yatakuwa kwenye mchezo huo kushuhudia wabongo wanaokipiga kwenye ligi hiyo nini watakachokifanya baada ya kuwa na muendelezo mzuri kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Asia.

Kwenye eneo la ushambuliaji Mbongo Clara Luvanda anaingia kwenye mchezo huo baada ya kuanza msimu kwa kasi, akifunga mabao saba katika ushindi wa  wa 12-0 dhidi ya CSKA Dushanbe kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Asia.

CLAR 01

Kwa ujumla kwenye mechi tatu za mashindano hayo Clara alifunga mabao tisa ,wastani wa kufunga mabao matatu kwa kila mechi.

Hata hivyo, safari ya Al Nassr kwenye Ligi ya Mabingwa Asia iliishia hatua ya awali licha ya ushindi huo mkubwa, baada ya kumaliza nyuma ya Bam Khatoon ya Iran.

Sasa Clara anageukia mashindano ya ndani akiwa na nafasi nyingine ya kuendelea kuonyesha kwa nini amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha mabingwa hao wa Saudi Arabia.

CLAR 02

Kibarua dhidi ya Al Ahli kinakuja baada ya Clara kumaliza msimu wa 2025/26 akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia akifunga mabao 24 na kuisaidia Al Nassr kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya nne mfululizo. Pia alitajwa kwenye kikosi bora cha msimu, jambo linaloonyesha mchango wake.

Mbali na Clara Mtanzania mwingine anayekipiga kwenye timu hiyo ni beki wa kati, Julietha Singano ambaye alijiunga na chama hilo msimu huu akitokea FC Juarez ya Mexico alikokuwa na kiwango bora.

Licha ya kujiunga hivi karibuni lakini beki huyo alicheza mechi zote tatu za mashindano ya Ligi ya Mabingwa Asia na kuonyesha uwezo mkubwa wa kuondoa hatari.