Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FOUNTAIN Gate Princess yasajili watatu Tausi

FOUNTAIN Pict

Muktasari:

  • Klabu hiyo imewasajili wachezaji watatu, Jamila Omari, Stella Wilbert Kwiligwa na Suzan Adam, ambao wote wametokea Tausi FC.

FOUNTAIN Gate Princess imeingia kambini ikijifua kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Wanawake huku ikiongeza nguvu kwenye kikosi chake.

Klabu hiyo imewasajili wachezaji watatu, Jamila Omari, Stella Wilbert Kwiligwa na Suzan Adam, ambao wote wametokea Tausi FC.

Jamila alijiunga Fountain Gate kwa mkopo wa miezi sita, baada ya Tausi FC kumruhusu kujiunga na klabu hiyo hadi Desemba mwaka huu, huku Stella amesaini kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Tausi FC.

Stella anayemudu kucheza nafasi ya kiungo, alikuwa nahodha wa kwanza wa Tausi FC kabla ya kuhamia Fountain Gate Princess, klabu ambayo aliwahi kuitumikia baada ya kuondoka Simba Queens.

Usajili mwingine ni wa Suzan Adam, ambaye naye amejiunga na Fountain Gate kama mchezaji huru baada ya kumaliza kwa mkataba wake na Tausi FC mwishoni mwa msimu uliopita.

Suzan, ambaye anacheza nafasi ya kiungo, anaifahamu vizuri Fountain Gate Princess kwani aliwahi kuitumikia kabla ya kuondoka kwenda Misri, ambako alicheza kwa misimu miwili.

“Ni wachezaji ambao tuna uhakika wanakwenda kuleta ushindani kwenye kikosi na hicho ndicho tunakitaka,” kilisema chanzo hiko.

Kurejea kwa Stella na Suzan kunaweza kuongeza uzoefu katika kikosi, kutokana na kuwa tayari wanaifahamu klabu hiyo, wakati Jamila akio ngeza chaguo jingine kwa benchi la ufundi.