Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Tanzania ilivyoendeleza uteja wa miaka nane kwa Azam FC

REKODI Pict

Muktasari:

  • Wanajeshi hao wameendeleza rekodi mbovu ya kutoshinda mechi yoyote ya Ligi Kuu dhidi ya Azam, tangu zilipoanza kukutana Oktoba 24, 2018.

USHINDI wa mabao 2-1 ilioupata Azam ikiwa ugenini dhidi ya JKT Tanzania, Oktoba 31, 2026, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar, umeendeleza rekodi mbovu ya Wanajeshi.

Wanajeshi hao wameendeleza rekodi mbovu ya kutoshinda mechi yoyote ya Ligi Kuu dhidi ya Azam, tangu zilipoanza kukutana Oktoba 24, 2018.

Ushindi wa Azam wa mabao hayo mawili yaliyofungwa na Idd Suleiman 'Nado' dakika ya 29 na lile la Lusajo Mwaikenda kwa kichwa, umeifanya JKT kushindwa kutamba nyumbani na kufikisha miaka nane sasa bila kuonja ushindi dhidi ya Azam.

JK 01

Katika mechi 13 walizokutana tangu mwaka 2018, Azam imeshinda mara tisa, huku nnne zikiisha kwa sare. JKT ikiwa haijaonja ushindi.

Tangu Oktoba 24, 2018 hadi Oktoba 31, JKT imefikisha siku 2,929 bila kuifunga Azam, sawa na miaka nane na siku saba tangu zilipokutana kwa mara ya kwanza.

Kinachozidi kuonyesha ukubwa wa rekodi hiyo ni namna Azam ilivyokuwa ikipata matokeo hata inapokutana na JKT kwenye uwanja wao. Mfano ni ushindi wa mabao 2-0 (Mei 21, 2024), kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, pamoja na ushindi wa bao 1-0 (Aprili 16, 2021). Hata katika mechi ya Oktoba 31, 2026, Azam imeondoka na pointi zote tatu ikiwa ugenini.

JK 02

Katika mechi hizo 13, Azam imefanikiwa kufunga mabao 25 dhidi ya nane ya JKT Tanzania, tofauti ya mabao 17. Ushindi wake mkubwa zaidi katika mechi hizo ulikuwa wa mabao 6-1 (Machi 8, 2019), wakati JKT ikiendelea kupata wakati mgumu.

Hata hivyo, JKT imekuwa ikionyesha nyakati za kupambana na Azam bila kuruhusu matokeo yawe upande wa wapinzani. Hilo linaonekana kupitia sare nne walizopata, ikiwemo ya mabao 2-2 (Desemba 1, 2019), sare ya bao 1-1 (Oktoba 30, 2020), 0-0 (Agosti 28, 2024) na 1-1 (Oktoba 1, 2025).

JK 03

Nahodha wa Azam ambaye aliibuka kuwa Mchezaji Bora wa mechi hiyo ya juzi, Lusajo Mwaikenda, amesema: "Ukiangalia JKT inapokuwa uwanja wa nyumbani inakuwa mechi ngumu kwa wapinzani, tulianza mechi tukiwa chini baada ya kuruhusu bao tukaenda mapumziko tukiwa sare ya 1-1 kipindi cha pili tulipambana tukapata bao.

"Tunajua uwanja huu miaka miwili sasa hatujapata pointi tatu, tumekuwa tukigawana pointi, kwahiyo hizi alama tatu zinamaana kubwa kwetu na kwa mashabiki wetu."