Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Mayanga awafunika wazawa

MAYANGA Pict

Muktasari:

  • Mbeya City ilianza msimu kwa kuchapwa bao 1-0 na Geita Gold, Agosti 14, 2026, kisha ikaifunga Dodoma Jiji mabao 2-0, Agosti 19, 2026, ikaichapa Mashujaa 2-1, Agosti 23, 2026 na ikashinda 2-0 mbele ya Fountain Gate, Agosti 28, 2026.

KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Salum Mayanga amekuwa kocha wa kwanza mzawa katika Ligi Kuu Bara msimu huu katika raundi nne kushinda mechi tatu mfululizo, akiwafunika wenzake wanane waliobaki.

Mbeya City ilianza msimu kwa kuchapwa bao 1-0 na Geita Gold, Agosti 14, 2026, kisha ikaifunga Dodoma Jiji mabao 2-0, Agosti 19, 2026, ikaichapa Mashujaa 2-1, Agosti 23, 2026 na ikashinda 2-0 mbele ya Fountain Gate, Agosti 28, 2026.

Amani Josiah wa Mashujaa FC, ameshinda mechi mbili bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, Agosti 15, 2026 na 2-1, mbele ya Kagera Sugar, Agosti 27, 2026, huku akichapwa 1-0 na Fountain Gate, Agosti 18, 2026, kisha 2-1 na Mbeya City, Agosti 23, 2026.

MAYA 01

Kocha Zubery Katwila wa Geita Gold, aliyeifunga Mbeya City bao 1-0, Agosti 14, 2026 na 6-2 dhidi ya Kagera Sugar, Agosti 22, 2026, akichapwa 1-0 na Namungo FC, Agosti 18, 2026 na akitoka sare ya 2-2 na Azam FC, Agosti 28, 2026.

Juma Mgunda wa Namungo FC, aliifunga Geita Gold bao 1-0, Agosti 18, 2026 na 1-0 dhidi ya Fountain Gate, Agosti 25, 2026, huku akichapwa na Yanga mabao 3-1, Agosti 15, 2026, kisha kuchapwa na JKT Tanzania 2-1, Agosti 29, 2026.

Mbwana Makata wa Polisi Tanzania, alianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC, Agosti 15, 2026, akaifunga JKT Tanzania 2-0, Agosti 20, 2026 na Dodoma Jiji 1-0, Agosti 25, 2026, kisha kuchapwa na Singida Black Stars 4-2, Agosti 29, 2026.

MAYA 02

Fredy Felix ‘Minziro’ wa Fountain Gate ameshinda mechi moja kwa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa FC, Agosti 18, 2026, akapoteza mechi tatu kwa kipigo cha 3-0 dhidi ya Singida Black Stars, Agosti 14, 2026, 1-0 na Namungo FC, Agosti 25, 2026 na 2-0 na Mbeya City, Agosti 28, 2026.

Ahmad Ally wa JKT Tanzania ameshinda moja ya mabao 2-1 dhidi ya Namungo FC, Agosti 29, 2026, akatoka sare ya 1-1 na TRA United, Agosti 16, 2026, kisha akachapwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania, Agosti 20, 2026 na 4-0 na Yanga, Agosti 24, 2026.

Kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias ametoa sare moja ya 1-1 dhidi ya TRA United, Agosti 24, 2026, kisha kuchapwa 1-0 na Mashujaa FC, Agosti 15, 2026, kichapo cha 4-1 dhidi ya Yanga, Agosti 20, 2026, akachapwa 1-0 na Simba, Agosti 27, 2026.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Juma Kaseja ametoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida Black Stars, Agosti 19, 2026, akachapwa 2-0 na Simba, Agosti 16, 2026, kipigo cha 6-2 kutoka kwa Geita Gold, Agosti 22, 2026, na 2-1 mbele ya Mashujaa, Agosti 27, 2026.

Katika makocha tisa wazawa wanaofundisha timu za Ligi Kuu Bara msimu huu 2026-2027, ni wawili tu ambao hawajashinda mechi yoyote hadi, ambao ni Fikiri Elias wa Coastal Union na Juma Kaseja wa Kagera Sugar.

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Salum Mayanga amesema kushinda mechi tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya msimu huu sio jambo jepesi kutokana na ushindani mkubwa uliopo, ingawa pongezi zaidi ni kwa wachezaji ambao wanafuata maelekezo yake vizuri.