Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa aipa miezi sita GGML kukamilisha ujenzi uwanja wa mpira Geita

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameipa miezi sita Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Magogo, unaojenhwa mkoani Geita.

Uwanja huo unajengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kushirikiana na kampuni hiyo kupitia Mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR). Kampuni hiyo ni wadhamini wakuu wa Timu ya Mpira ya Geita Gold Mine inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Majaliwa alitoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya madini kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania (TMIF) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Majaliwa ambaye alifunga mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, alipata maelezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi anayeshughulikia mahusiano ya jamii kutoka GGML, Gilbert Mworia na kupongeza kazi kubwa inayofanywa na kampuni hiyo ikiwemo kuwa mdhamini mkuu wa mkutano huo.

“Tunawapongeza sana kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuzingatia matakwa ya sheria ya madini kuhusu kipengele hicho cha CSR, kwa mfano katika hili suala la ujenzi wa uwanja wa mpira Magogo mnatakiwa kumalizia kulitekeleza haraka ndani ya miezi sita,” alisema Majaliwa

“Lakini pia msiangalie kujenga uwanja mkoani Geita peke yake, mmpeleke huduma hizi na mikoa mingine ili ifaidike na kukuza vipaji vya vijana wetu,” alisema Majaliwa.

Awali, akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Mworia alisema kampuni hiyo imekuwa kinara katika kuzingatia masuala ya uhifadhi wa mazingira, afya na usalama mahala pa kazi.

Mworia alisema GGML imeendelea kuwa mfano wa kuigwa nchini kutokana na kuzingatia suala la afya na usalama mahala pa kazi hali iliyoifanya kampuni hiyo kushinda mara nne mfululizo tuzo hiyo inayotolewa na kampuni mama ya AngloGold Ashanti na kuishinda migodi mingine duniani.

Kuhusu ujenzi wa uwanja huo wa mpira, Mworia alimhakikishia waziri mkuu ndani ya miezi sita utakuwa umekamilika lakini pia wataandaa mpango wa kutoa mchango katika sekta hiyo kwenye mikoa mingine.

Hata hivyo, akifunga maonesho hayo, Majaliwa alisema Serikali itaendelea kuipa umuhimu sekta ya madini ilikuwa injini ya uchumi wa Taifa.

Alisema Serikali ipo tayari na inaruhusu miradi ya maendeleo kutoka Sekta binafsi katika Utafutaji, Uchimbaji, uchorongaji na uongezaji thamani madini ili kufanikisha mikakati iliyopo kwa wachimbaji kwa wachimbaji wote nchini.

Naye Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alisema wizara imetumia mkutano huo katika kukuza ushirikiano wa kikazi baina ya nchi na nchi kupitia mada mbalimbali zilizowasilishwa kama vile majadiliano kuhusu matumizi ya nishati safi ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema kwa mwaka 2023 mchango wa wachimbaji katika sekta madini ilikusanya Sh bilioni 678 sawa na asilimia 40 ya makusanyo yote hali inayoonesha sekta hiyo kupiga hatua.