Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makosa ya kipa yaigharimu Mafunzo

MAFUNZO Pict

Muktasari:

  • Kipa huyo alionekana kuvurugika baada ya kosa hilo na muda mfupi baadaye Yazidu Iddi akaongeza bao la pili na kuipa Raskazone ushindi. Mafunzo imecheza mechi saba bila ushindi, ikipata sare nne na kupoteza michezo mitatu.

MAKOSA ya kipa Ali Athumani, yameigharimu Mafunzo baada ya timu hiyo kuendelea na mfululizo wa matokeo mabaya katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Mafunzo ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Raskazone katika mchezo uliochezwa Oktoba 2, 2026, huku bao la kwanza likitokana na kosa la kipa huyo.

Wakati Raskazone ikisaka bao la kuongoza baada ya timu hizo kwenda mapumziko bila kufungana, Ali alitoka katika eneo lake la ulinzi na kutoa nafasi kwa wapinzani wake kutumia udhaifu huo.

Katika hali hiyo ya vuta nikuvute, Hafidh Omar alimsoma kipa huyo na kuachia shuti la mbali lililomshinda Ali, ambaye alibaki akilitazama likiingia wavuni.

Kipa huyo alionekana kuvurugika baada ya kosa hilo na muda mfupi baadaye Yazidu Iddi akaongeza bao la pili na kuipa Raskazone ushindi. Mafunzo imecheza mechi saba bila ushindi, ikipata sare nne na kupoteza michezo mitatu.