Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Maria Nyerere awapa baraka washiriki wa Vodacom Nyerere Cycling Tour

NYERERE Pict

Muktasari:

  • Mama Maria alitoa baraka hizo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipokutana na waendesha baiskeli wa msafara huo, ambao walikwenda kumuaga kabla ya kuanza safari kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara.

Mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere, amewabariki waendesha baiskeli wanaoshiriki Nyerere Cycling Tour, safari inayolenga kuunganisha mchezo huo na shughuli za kijamii.

Mama Maria alitoa baraka hizo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipokutana na waendesha baiskeli wa msafara huo, ambao walikwenda kumuaga kabla ya kuanza safari kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara.

NYERE 0004
NYERE 0004

Safari hiyo, inayofanyika sambamba na mashindano ya Vodacom Coastal Classic, imeandaliwa kwa lengo la kutumia mchezo wa baiskeli kama chombo cha kuhamasisha na kuchangia maendeleo ya jamii.

NYERE 01

Mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere (katikati) akizungumza mara baada ya kukutana na waendesha baiskeli wa msafara wa Nyerere Cycling Tour ambapo wadhamini wakuu wa msafara huo kampuni ya Vodacom Tanzania PLC waliokwenda kumuaga na kupata baraka zake kabla ya kufanya mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na Nyerere Cycling Tour.

Kupitia Nyerere Cycling Tour, waandaaji na washirika wake wanatarajia kutekeleza shughuli mbalimbali katika maeneo yatakayopitiwa na msafara huo, zikiwemo elimu, afya, uhifadhi wa mazingira, elimu ya fedha na maendeleo ya jamii.

Miongoni mwa mipango hiyo ni kutoa madawati 1,000, kujenga madarasa 10, kukarabati madarasa 40 na kupanda miti, huku shughuli hizo zikitarajiwa kuwafikia zaidi ya watu 25,000.

NYERE 02

Meneja Mauzo na mkakati wa biashara wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania Plc, Caleb Majo akizungumza na waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour wakati wa hafla ya kuwaaga na kupata baraka kutoka kwa Mama Maria Nyerere kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara.

Akizungumza baada ya kukutana na waendesha baiskeli hao, Mama Maria aliwatakia safari njema na kuwatia moyo katika jukumu hilo linalolenga kuenzi urithi wa Mwalimu Nyerere huku likitumia michezo kugusa maisha ya wananchi.

Msafara huo unaungwa mkono na wadau mbalimbali, akiwemo mdhamini mkuu, Vodacom Tanzania PLC, ambao walishiriki katika kuwaaga waendesha baiskeli hao kabla ya safari.

NYERE 04

Mtoto wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Madaraka Nyerere akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour na kutoa salamu za familia ya Mwalimu Nyerere. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania PLC, Caleb Majo, mtoto wa Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere, na Mkuu wa Kitengo cha Tahadhari wa Stanbic Bank Tanzania, Wilmot Ishengoma, pamoja na wadau wengine wa mchezo wa baiskeli.

Safari ya Nyerere Cycling Tour inaweka msisitizo kwenye nafasi ya michezo katika kuhamasisha shughuli za maendeleo, huku waendesha baiskeli wakitarajiwa kuwa sehemu ya ujumbe wa kuenzi historia ya Mwalimu Nyerere na kuchochea mabadiliko chanya katika jamii.

NYERE 003
NYERE 003