Manara: Naweka nguvu zangu Yanga

BAADA ya kutambulishwa na uongozi wa Yanga, aliyekuwa ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema nguvu alizokuwa anazitumia Simba amezihamishia kwa mabosi wake wapya.
Manara amesema alikuwa anatumia nguvu nyingi Simba lakini wakawa wanamchukulia kawaida na nguvu hizo zitaanza kuonekana.
SOMA: Manara rasmi Yanga
“Wapo wanasema ni klabu kubwa, hayo yote hayawezi kuwezekana kama hakuna watu hivyo vyote haviwezekani,” anasema Manara.
Manara amesema kuwa Yanga ni kama hisani kwa sababu viongozi wote wa klabu hiyo wanajua nilikuwa Simba.
SOME: Manara: Sikuwa na namna
“Nimevaa jezi ya Yanga na nimeambatana na familia yangu yote nawashukuru sana kwa kuniunga mkono hata huku nilipokuja, nimevaa jezi ya Yanga na sasa nipo huku,” anasema Manara.