Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Singida Black Stars wawekwa mtegoni

SINGIDA Pict

Muktasari:

  • Nyota mwingine aliyefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mkataba wake ni Dramane Kambou raia wa Burkina Faso, ambaye tangu amejiunga na timu hiyo akitokea FC Saint-Eloi Lupopo ya DR Congo ameshindwa kuonyesha ushindani kikosini.

HALI si shwari kwa mastaa wa Singida Black Stars ambao wana kazi kubwa ya kuboresha viwango ili kuepuka panga linalokuja mbele wakati dirisha dogo la usajili linapotarajiwa kufunguliwa Januari 2027.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza wachezaji waliokalia kuti kavu ni wale watakaoshindwa kuonyesha viwango vizuri kuanzia sasa, jambo ambalo tathimini ya kina imeanza chini ya benchi la ufundi.

Chanzo kimeliambia Mwanaspoti kwamba, benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkongomani Papy Kimoto, limeanza kufanyia tathimini mchezaji mmoja mmoja, kwa kuzingatia pia mahitaji ya kikosi hicho kwa msimu huu.

SINGI 02

“Hadi kufikia usajili wa dirisha dogo Januari 2027, tutakuwa tumefikia uamuzi wa mwisho, tathimini tumeianza mapema na tutaanza kuizingatia mechi za Ligi Kuu na za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilisema benchi la ufundi limepewa nafasi ya kufanyia tathimini kila mchezaji, jambo ambalo limeanza mapema na ndio sababu baadhi yao wameomba kuvunja mikataba yao kutokana na kushindwa kupigania nafasi ndani ya kikosi hicho.

Kwa upande wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa Singida, Hussein Massanza amesema maboresho yanayoendelea ni kutokana na mahitaji ya timu hiyo, ndio maana baadhi yao wameamua kusitisha mikataba yao, kwa sababu ya kuona ushindani kikosini.

SINGI 01

Wachezaji ambao tayari wameondoka ni kiungo raia wa Austria, Marcel Canadi aliyejiunga msimu huu akitokea Enosis Neon Paralimni ya Cyprus, Mohamed Damaro wa Guinea na winga Ladack Chasambi.

Nyota mwingine aliyefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mkataba wake ni Dramane Kambou raia wa Burkina Faso, ambaye tangu amejiunga na timu hiyo akitokea FC Saint-Eloi Lupopo ya DR Congo ameshindwa kuonyesha ushindani kikosini.