Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda ataja mambo mawili Namungo FC

Muktasari:

  • Namungo FC imeshacheza jumla ya mechi sita hadi sasa na imepata ushindi mara mbili na kupoteza mechi nne. Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kuwa na pointi sita.

KOCHA Juma Mgunda amesema kutotumia vizuri nafasi wanazotengeneza katika safu ya ushambuliaji, pamoja na kufanya makosa katika eneo la ulinzi, ni miongoni mwa sababu kubwa zinazowagharimu na kuwafanya kupoteza pointi katika mechi zao za Ligi Kuu Bara.

Namungo FC imeshacheza jumla ya mechi sita hadi sasa na imepata ushindi mara mbili na kupoteza mechi nne. Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kuwa na pointi sita.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mgunda ambaye juzi timu yake ilichapwa na Dodoma bao 1-0 alisema wamebaini upungufu huo na sasa wameanza kufanya kazi kwa kina, huku akisisitiza umuhimu wa wachezaji kuongeza umakini katika maeneo yote mawili. “Tumeliona hilo, hasa katika kutumia nafasi tunazopata, pamoja na makosa katika eneo la ulinzi. Haya ni mambo ambayo tunakwenda kuyafanyia kazi ili kuhakikisha yanarekebishika,” alisema Mgunda.

Kocha huyo alisema changamoto kubwa zaidi imekuwa ni baadhi ya makosa kujirudia mara kwa mara, hali ambayo imekuwa ikiwafanya kupoteza umakini katika nyakati muhimu za mchezo na hatimaye kuangusha pointi.

“Makosa mengi yamekuwa yakijirudia sana. Tunapoteza umakini katika baadhi ya nyakati na mwisho wake tunajikuta tumeangusha pointi ambazo tulipaswa kuzichukua,” alisema.

Mgunda aliongeza kwa sasa jambo kubwa ni kuhakikisha wachezaji wanaelewa maeneo ambayo wamekuwa wakikosea na kuyafanyia kazi katika mazoezi, ili timu iwe na umakini zaidi katika mechi zi-jazo.

“Kikosi chetu hakiwezi kumudu kuendelea kupoteza pointi kutokana na makosa ambayo yanaweza kurekebishwa. Hivyo, nidhamu na umakini zaidi katika safu ya ushambuliaji na ulinzi vinahitajika,” alisema.

Namungo FC iliyopo nafasi ya 11 na pointi sita baada ya mechi saba, inatarajiwa kushuka dimbani katika mchezo wake ujao dhidi ya TRA United, uliopangwa kuchezwa Alhamisi, Oktoba 8, 2026, katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.