Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mmesikia huko….Yanga hii ndo kwaanza

New Content Item (1)
MWENYEKITI wa Yanga, Dk Mshindo Msolla

Muktasari:

MWENYEKITI wa Yanga, Dk Mshindo Msolla amewaambia mashabiki kwamba ndio kwanza gari limepata moto. Dk Msolla ambaye pia kitaaluma ni Kocha amesisitiza kwamba duru lijalo moto wao hautazuilika.

MWENYEKITI wa Yanga, Dk Mshindo Msolla amewaambia mashabiki kwamba ndio kwanza gari limepata moto. Dk Msolla ambaye pia kitaaluma ni Kocha amesisitiza kwamba duru lijalo moto wao hautazuilika.

Yanga imemaliza kibabe mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ikiwa kileleni mwa msimamo ikishinda mechi zao 13 kati ya 17 na zilizobaki ni sare na hawajapoteza mechi.

Rekodi hiyo imemuibua Mwenyekiti huyo msomi, aliyesema wakati wa mapumziko ya kupisha michuano ya CHAN na Kombe la Mapinduzi wanaamini kocha wao, Cedric Kaze atakuwa na muda wa kutosha zaidi kuingiza mbinu zake na kuzidi kuweka uimara wa kikosi chao.

“Nikizungumza kwa uelewa wangu kama kocha wa soka,inawezekana tukafanya vizuri zaidi katika mzunguko wa pili kwani katika duru hili la kwanza kocha wetu (Cedric Kaze) aliukuta katikati lakini amepambana kuingiza ubora na sasa tuko hivi,” alisema Dk Msolla ambaye huzungumza kwa nadra sana.

“Sasa hivi kocha timu ameshaielewa wachezaji nao wamemjua kocha wao na wanatambua nini kocha anakitaka kwenye yale mapumziko ya mashindano ya Chan na Mapinduzi ukiondoa mchezo wa Prisons tutakuwa na timu bora na ngumu zaidi ambayo itakuwa na ubora mkubwa wa kucheza kama timu.

“Kama uongozi tunaridhika sana na kazi inayofanywana makocha wetu kuanzia mkuu wao Kaze lakini pia ubora mkubwa wanaouonyesha wachezaji wetu katika mechi zote 17 walizocheza mpaka sasa,” alisema.

Aidha Dk Msolla aliwataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kufurika katika kila mchezo ambao wanacheza ambapo hali hiyo ya kujaa viwanja imekuwa ikiwapa hamasa wachezaji wao kujituma zaidi. “Nipo ndani ya uongozi kuna mambo matatu lazima tuwapongeze wenzetu wa GSM kwa kazi yao kubwa hasa Mwenyekiti wao Ghalib Mohamed, hatua yao ya kwanza kuamua kusajili hii timu ndio kitu muhimu kwetu kama Yanga kuwa na timu bora.

“Wakati tunawaacha wachezaji baadhi wakubwa wengi walishangaa na kutuona tunaharibu lakini ujio wa wachezaji wapya ambao wana ubora mkubwa ndio sasa unadhihirisha ukomavu wa maamuzi tuliyofanya.

“Hatua ya pili ametusaidia kuiweka timu kambini sehemu ambayo ina hadhi na wachezaji wakafanya mazoezi kwa kiwango bora, mazingira sahihi ya mchezaji anayofanyia maandalizi yamempa utulivu wa kuweza kujiandaa vyema na mwisho ni katika kuwapa motisha wachezaji.

“Hivi sasa mchezaji hapa Yanga lazima ajitume kwani anajua akishinda kuna kitu kikubwa anakuja kupata lakini pia mashabiki wetu nao wamekuwa nyuma na timu yao kila inapokwenda kila uwanja Yanga inapocheza inajaza hata kama wako ugenini unaona asilimia 80 ya mashabiki ni wao.

“Utatu huu kwa pamoja ndio umekuwa silaha muhimu kwetu hivyo kwa mazingira kama haya na kama tutazidisha umoja naamini kuna mambo makubwa zaidi yanakuja mzunguko wa pili kwqa kuendelea kushinda kwa kishindo kwa kuwa timu bora tunayo,” alisema Dk Msolla.

YANGA PRINCESS

Dk Msolla pia aliipongeza timu yao ya wanawake ,Yanga Princess inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) akisema kuamua kusajili mastaa hata katika kikosi hicho sambamba na malezi mazuri yamechangia kutisha msimu huu.

Yanga Princess nao hawajapoteza mechi yoyote katika mechi 6 wakifikisha pointi 16 wakitoa sare moja pekee na hawajapoteza mchezo wowote.

“Watu wanaona hii timu ya wanaume tu, lakini kuna mkakati tuliupanga msimu huu, angalia ujio wa mchezaji bora kama Filomena (Daniel) na wengine, lakini acha hapo posho na matunzo mengine nao wanayapata kama kawaida msimu huu tulidhamiria kufanya makubwa haya,”alisema Kocha huyo wa zamani wa Milambo Tabora, Reli ya Morogoro na timu ya taifa, Taifa Stars miaka ya 2000 kabla ya kuchaguliwa Yanga.