Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrithi wa Edna Yanga Princess njiani kutua

EDNA Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa kikosi hicho kinamtazama kocha wa zamani wa Tausi FC, Mjerumani Martin Hammel ambaye alikuwepo jukwaani kwenye mechi ya mshindi wa tatu kati ya Yanga iliyoshinda kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Mashujaa Queens baada ya dakika 90 kutamatika kwa sare ya 1-1.

UONGOZI wa Yanga Princess umeanza rasmi mchakato wa kumsaka mrithi wa Kocha Edna Lema ambaye alijiondoa kikosini hapo baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya watani zao Simba Queens kwenye mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii kwa wanawake.

Inaelezwa kikosi hicho kinamtazama kocha wa zamani wa Tausi FC, Mjerumani Martin Hammel ambaye alikuwepo jukwaani kwenye mechi ya mshindi wa tatu kati ya Yanga iliyoshinda kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Mashujaa Queens baada ya dakika 90 kutamatika kwa sare ya 1-1.

Inaelezwa kuna asilimia kubwa kocha huyo akainoa timu hiyo msimu huu kutokana na viongozi kushawishika na ubora aliouonyesha kwenye kikosi cha Tausi ambayo ilipanda msimu kwa mara ya kwanza msimu uliopita na ikafanya vizuri.

Kocha huyo ambaye viongozi wa Yanga Princess wanaamini ana uwezo wa kuifundisha timu hiyo kutokana na uzoefu alioupata kwenye ligi hiyo na mbinu bora alizonazo kushindana na vigogo kama Simba na JKT.

ED 02

Kabla ya kuelekeza nguvu kwa Hammel ambaye aliisaidia Tausi kumaliza nafasi ya saba na pointi 24 msimu uliopita, taarifa za ndani kutoka Yanga Princess zilieleza kuwa chaguo la kwanza la viongozi lilikuwa ni Kocha Bakari Shime, ambaye kwa sasa anaifundisha Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ya U-20 (Tanzanite).

Hata hivyo, mpango wa kumng’oa Shime umeonekana kuwa na ugumu mkubwa kutokana na mkataba na majukumu yake ya sasa ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), jambo lililowalazimu mabosi wa Yanga kubadili mwelekeo kwa haraka.

ED 01

“Baada ya kocha kujiondoa viongozi wanaamini Hammel ana uwezo wa kuisaidia timu na uzuri ni kwamba ataanza na timu kwa sababu timu bado mpya,” kilisema chanzo cha ndani.

Yanga Princess inalenga kukamilisha mchakato huo mapema iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) 2026/2027, huku kwa sasa timu hiyo ikiwa chini ya Kocha wa muda, Said Maulid ‘SMG’, ambaye alikuwa msaidizi wa Edna Lema