Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nani kubeba ndoo Ligi Kuu ya Wanawake Bara?

NDOO Pict

Muktasari:

  • Tangu ligi hiyo ilipoanzishwa msimu wa 2016/17, Simba imekusanya mataji matano, JKT Queens ikifuata kwa mataji manne, huku Yanga Princess ikiwa bado haijafanikiwa kutwaa ubingwa.

SIMBA Queens, JKT Queens na Yanga Princess ni miongoni mwa timu zinazotarajiwa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara (WPL) msimu wa 2026/27 unaoanza leo, Oktoba l28, 2026 kutokana na ilichofanya ndani ya misimu minne iliyopita.

Lakini kwa mujibu wa rekodi na historia za msimu uliopita zinaweka Simba katika nafasi nzuri zaidi ya kutetea taji hilo baada ya ilichokifanya msimu uliopita na mwanzoni mwa msimu huu iliponyakua taji la Ngao ya Jamii kwa kuwafunga wapinzani wake Yanga Princess 3-0 na JKT 1-0.

Tangu ligi hiyo ilipoanzishwa msimu wa 2016/17, Simba imekusanya mataji matano, JKT Queens ikifuata kwa mataji manne, huku Yanga Princess ikiwa bado haijafanikiwa kutwaa ubingwa.

NDO 01

SIMBA IMETAWALA MARA TANO

Simba Queens ndiyo timu iliyotwaa ubingwa mara nyingi zaidi katika historia ya WPL. Ilianza kutawala kuanzia msimu wa 2019/20, ilipobeba taji lake la kwanza, kabla ya kuendeleza mafanikio hayo misimu miwili iliyofuata.

Simba ilitwaa mataji katika misimu ya 2019/20, 2020/21 na 2021/22, kisha ikarejea tena mwaka 2023/24 na kuongeza taji la tano msimu uliopita.

Katika kipindi hicho, timu hiyo imeonyesha uwezo wa kujenga kikosi kinachoweza kushindana kwa muda mrefu.

Hata ilipokosa ubingwa, iliendelea kuwa miongoni mwa timu zinazoweza kupambana hadi mwisho wa ligi.

Msimu wa 2025/26, Simba ilithibitisha ubora wake kwa kumaliza ligi bila kupoteza mchezo wowote kati ya mechi 22. Ilishinda mechi 19 na kutoka sare tatu, ikifunga mabao 52 na kuruhusu nane. Ilikusanya pointi 60.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa nguvu ya Simba haikuwa katika kufunga pekee, bali pia katika kuzuia wapinzani kupata mabao.


NDO 03

JKT HAIPO MBALI

JKT ndio mshindano mkubwa wa ubigwa kwa Simba Queens na inastahili kupewa heshima yake baada ya kutawala kwa misimu minne mataji ya ligi. Timu hiyo imetwaa mataji manne ya WPL misimu ya 2017/18, 2018/19, 2022/23 na 2024/25.

Rekodi hiyo inaonyesha kuwa JKT imekuwa mpinzani wa mara kwa mara katika mbio za ubingwa, hasa kutokana na uwezo wake wa kurejea kileleni baada ya kupitwa na wapinzani.

Msimu wa 2024/25, JKT ilitwaa ubingwa baada ya kumaliza ligi ikiwa na pointi 47 sawa na Simba Queens, lakini ikashinda kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Ilifunga 70 na kuruhusu saba, rekodi iliyoonyesha uimara wake mbele.

Hata hivyo, msimu wa 2025/26 uliipa JKT changamoto nyingine. Ilimaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi 46, nyuma ya Simba ilifunga mabao 46 na kuruhusu 10.

NDO 02

YANGA NA HISTORIA

Tofauti na wapinzani wake wawili, Yanga Princess bado haijawahi kubeba taji hilo. Msimu wa 2020/21, Yanga ilimaliza ikiwaya pili nyuma ya Simba, ikiwa imepoteza ubingwa kwa tofauti ya pointi moja tu.

Katika msimu wa 2025/26, ilimaliza tena nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50, ikifunga mabao 56 na kuruhusu 16.

Takwimu za msimu uliopita zinaonyesha kuwa Yanga ilikuwa na uwezo mkubwa wa kushambulia kuliko hata Simba kwa idadi ya mabao, lakini iliruhusu mabao mengi zaidi na kukusanya pointi chache.

Ikiwa itaimarisha safu ya ulinzi na kudumisha uwezo wake wa kutengeneza nafasi za kufunga, inaweza kupunguza pengo lililokuwepo.

Changamoto yake kubwa itakuwa kugeuza uwezo huo kuwa ushindi mfululizo, hasa katika michezo inayoweza kuamua hatima ya ubingwa.


NANI ANA NAFASI?

Kwa kuzingatia takwimu 2025/26, Simba Queens  inaingia kwenye msimu mpya ikiwa na rekodi bora zaidi ya matokeo. Kutopoteza mchezo wowote, kukusanya pointi 60 na kuruhusu mabao nane pekee ni viashiria vinavyoonyesha uimara wake. JKT Queens ina uzoefu wa kutwaa mataji na tayari imethibitisha kuwa inaweza kushindana na Simba katika mbio za ubingwa. Yanga Princess nayo ina uwezo wa kufunga mabao mengi, lakini inahitaji kuboresha eneo la mabeki.

Kwa sasa, Simba inaanza ikiwa na faida ya rekodi ya hivi karibuni, huku JKT ikiwa na historia ya kutwaa mataji na Yanga ikiwa na nafasi ya kuandika ukurasa mpya. Jibu la nani atabeba ubingwa litapatikana baada ya ligi kuamua ndani ya uwanja.