Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu ya Wanawake kazi leo

WPL Pict

Muktasari:

  • Simba itaanza safari ya kutetea taji lake kwa kucheza na Kilimanjaro Wonders kwenye Uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro, mchezo unaotarajiwa kuwa kipimo cha kwanza kwa timu hizo kwenye malengo yao ya msimu huu.

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania (WPL) msimu wa 2026/2027 inaanza leo Oktoba 28 2026, kwa mechi sita zitakazoanza saa 10 jioni, huku macho yakielekezwa kwa bingwa mtetezi Simba Queens na timu zilizopanda daraja msimu huu.

Simba itaanza safari ya kutetea taji lake kwa kucheza na Kilimanjaro Wonders kwenye Uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro, mchezo unaotarajiwa kuwa kipimo cha kwanza kwa timu hizo kwenye malengo yao ya msimu huu.

Mchezo mwingine utakaokuwa na mvuto ni kati ya Yanga Princess ambaye msimu uliuopita ilimaliza nafasi ya tatu itakayovaana na Bunda Girls utakaochezwa Uwanja wa Karume Ilala, jijini Dar es Salaam.

UFU 01

Bunda Girls imepanda daraja kutoka ligi ya mkoa na sasa inakutana na moja ya timu zinazofanya vizuri katika soka la wanawake Tanzania.

Katika michezo mingine ya raundi ya kwanza, Fountain Gate Princess itakutana na Mashujaa Queens Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Geita Queens itaumana na JKT Queens kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Geita, huku Ceasiaa Queens ikipambana na Alliance Girls kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

UFU 02

Mchezo wa sita utazikutanisha Tausi FC na Bunda Queens kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na timu hizo zitakuwa na nafasi ya kuanza msimu kwa matokeo mazuri na kujiweka katika mazingira bora ya kuwania malengo yao.