Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dabi za moto WPL, Kariakoo usiseme!

DABI Pict

Muktasari:

  • Dabi hizo ni kutoka Kanda ya Ziwa, ambako Bunda Queens itakutana na Bunda Girls, hadi kwenye pambano la timu za kijeshi la Mashujaa Queens na JKT Queens, kisha Kariakoo Dabi kati ya Simba Queens na Yanga Princes.

WAKATI Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (WPL) msimu wa 2026/27 ikianza safari ya kutafuta bingwa mpya, macho ya mashabiki hayatakuwa kwenye mbio za ubingwa pekee, bali pia kwenye dabi zinazotarajiwa kuongeza joto la ushindani katika ligi hiyo.

Dabi hizo ni kutoka Kanda ya Ziwa, ambako Bunda Queens itakutana na Bunda Girls, hadi kwenye pambano la timu za kijeshi la Mashujaa Queens na JKT Queens, kisha Kariakoo Dabi kati ya Simba Queens na Yanga Princes.

Hizi ni baadhi ya dabi zinazotarajiwa kuwa na ushindani msimu huu, kwa kuzingatia historia ya timu hizo na matokeo ya mikutano yao iliyopita.


DAB 04

DABI YA KARIAKOO

Hii ndiyo dabi inayobeba historia ndefu zaidi kati ya zilizotajwa, ikiwa ni pambano la Simba Queens na Yanga Princess, timu ambazo zimekuwa zikikutana katika michezo yenye ushindani wa kuwania ubora wa soka la wanawake nchini.

Katika Ngao ya Jamii iliyotajwa kwenye maandalizi ya msimu huu, Simba Queens iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Yanga Princess, matokeo yaliyoongeza hamasa kabla ya ligi kuendelea.

Ukiangalia timu hizo zimekutana mara 15 kwenye ligi kuanzia msimu wa 2019/20 hadi 2025/26, Simba imeshinda mara 10, Yanga mara mbili, huku michezo mitatu ikiisha kwa sare. Katika kipindi hicho, Simba imefunga mabao 37 dhidi ya 10 ya Yanga.

Msimu wa 2019/20, kwenye dabi ya kwanza ya kihistoria iliyopigwa Uwanja wa Karume Januari 13, 2019 Simba ilishinda kwa mabao 7-0 huku Mwanahamisi Omary akigeuka kuwa mwiba baada ya kufunga mabao manne mengine yakifungwa na Amina Bilal, Amina Ramadhani waliofunga moja moja na lingine likiwekwa kambani na Frola Kayanda aliyejifuna kwa upande wa Yanga.

Desemba 14, 2019 Simba ilipata ushindi wa mabao 3-1, kisha ikaongeza ushindi wa 5-1 Julai 11, 2020. Msimu uliofuata, timu hizo zilitoka sare ya 0-0 kabla ya Simba kushinda 3-0 katika mchezo mwingine.

Msimu wa 2021/22, Simba ilishinda 4-1 katika mchezo wa kwanza, lakini Yanga ikajibu kwa ushindi wa bao 1-0. Msimu uliofuata, timu hizo zilitoka sare mbili za mabao 1-1, matokeo yaliyoonyesha kuwa Yanga iliweza kuzuia ushindi wa mpinzani wake.

Katika msimu wa 2023/24, Simba ilishinda michezo yote miwili kwa mabao 3-1 na 3-1, kabla ya timu hizo kugawana ushindi msimu wa 2024/25. Yanga ilishinda 1-0 katika mchezo mmoja, lakini Simba ikajibu kwa ushindi wa bao 1-0 katika mwingine.

Msimu uliopita, Simba iliendeleza matokeo mazuri kwa kushinda 2-0 katika mchezo wa Desemba 28, 2025, kisha ikaifunga Yanga 2-1 Mei 15, 2026.

Hata hivyo, licha ya takwimu hizo kuipa Simba rekodi nzuri katika mechi za ligi.


DAB 01

BUNDA KWA BUNDA

Ukiachana na mbio za ubingwa ambazo zitakuwa zikiangaliwa kwa ukaribu mechi nyingine ni hii dabi ya kanda ya Ziwa.

Pambano la Bunda Queens dhidi ya Bunda Girls linaweza kuwa miongoni mwa michezo yenye mvuto wa kipekee, likizikutanisha timu zinazotoka eneo moja la Kanda ya Ziwa.

Bunda Girls inaingia kwenye ushindani wa ligi kuu baada ya kupanda daraja kutoka ligi ya mkoa, hatua inayoweka mazingira ya kukutana na Bunda Queens katika pambano linaloweza kuwa na ladha ya kipekee kwa mashabiki wa soka la wanawake wa eneo hilo.

DAB 02

Mechi za aina hii, ushindani hauishii kwenye pointi tatu pekee. Pia ni nafasi ya timu kujipambanua mbele ya mashabiki wa eneo moja na kuonyesha ubora wake dhidi ya mpinzani anayeifahamu mazingira yake.


DAB 03

MASHUJAA VS JKT

Dabi nyingine inayotarajiwa kuvutia macho ni kati ya Mashujaa Queens na JKT Queens, timu mbili zinazohusishwa na taasisi za kijeshi.

Timu hizo zimekuwa na historia tangu Mashujaa ilianza rasmi kucheza mashindano ya ligi msimu wa 2024/25, baada ya kubadilishwa jina la timu iliyokuwa ikijulikana kama Amani.

Kwa mujibu wa rekodi timu hizo zimekutana mara nne, Mashujaa Queens haijapata ushindi dhidi ya JKT Queens. JKT imeshinda michezo mitatu, huku mchezo mwingine ukiisha kwa suluhu ya bila kufungana.

DAB 05

Takwimu hizo zinaweka wazi changamoto inayomkabili Mashujaa katika kujaribu kubadili rekodi hiyo msimu huu. Kwa upande wa JKT, historia hiyo ni kumbukumbu nzuri.

Mashujaa itahitaji kuingia uwanjani ikiwa na mpango wa kuvunja uimara wa mpinzani wake, wakati JKT itakuwa na jukumu la kuthibitisha kuwa inaweza kuendeleza matokeo mazuri dhidi ya timu hiyo.


MSIMU WA DABI

Kwa ujumla, dabi zinaongeza mvuto wa WPL 2026/27; Bunda Queens na Bunda Girls zinakutana katika pambano la eneo moja, Mashujaa Queens na JKT Queens zinapimana nguvu katika dabi ya timu za jeshi, huku Simba Queens na Yanga Princess zikiendeleza ushindani Kariakoo.

Mashabiki watasubiri kuona kama Simba itaendelea kutawala Kariakoo Dabi, kama Mashujaa itavunja rekodi dhidi ya JKT, na namna Bunda Girls itakavyojipambanua katika Ligi Kuu.