Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Azam FC alia na ugumu Ligi Kuu

STAR Pict

Muktasari:

  • Molia alifunga bao la kwanza dakika ya 24 kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, iliyochezwa Agosti 23, 2026.

BAADA ya kufunga bao lake la kwanza kwenye mechi dhidi ya Pamba Jiji, winga wa Azam, Henock Molia ameshindwa kuzuia furaha yake, huku akitaja Ligi ya Tanzania kuwa ni miongoni mwa mashindano magumu.

Molia alifunga bao la kwanza dakika ya 24 kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, iliyochezwa Agosti 23, 2026.

Mkongomani huyo mwenye uwezo wa kucheza kama winga wa kulia au kushoto, alitua Azam FC mwezi Julai 2026 kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya nchini DR Congo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Molia amesema licha ya kucheza mechi tatu pekee tangu aanze kuitumikia timu hiyo, tayari ameshaanza kupata picha ya ushindani uliopo kwenye Ligi ya Tanzania, akisisitiza kiwango cha ligi hiyo si cha kubeza na kinahitaji maandalizi makubwa kwa mchezaji.

STA 01

“Baada ya kucheza mechi tatu nimegundua ligi ya Tanzania ni ngumu. Inahitaji kujituma na kujiimarisha zaidi kwa nguvu, hivyo bado nina kazi kubwa ya kufanya ili niweze kuendana na ushindani uliopo,” amesema Molia.

Mkongomani huyo msimu uliopita aliimbwa sana akiwa kwao DR Congo akifunga mabao 11 na 10 ni katika ligi na bao moja Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akitoa asisti tisa.

Amesema amefurahia kuanza kuifungia Azam, akieleza hatua hiyo imempa morali ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuongeza idadi ya mabao katika mechi zijazo.

Ameongeza kuwa, bao hilo ni mwanzo mzuri kwake na limempa kujiamini zaidi katika kuendelea kutafuta mabao na kusaidia timu kupata matokeo mazuri.

STA 02

“Nimefurahia sana kuanza kufunga kwa sababu ni kitu ambacho kinanipa morali kubwa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi. Nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii kwenye mazoezi na kwenye kila mchezo, hivyo kupata bao hili kunanipa nguvu na kujiamini zaidi.

“Nataka kuendelea kujituma, ili kuongeza kiwango changu na kuhakikisha kila nafasi nitakayoipata naitumia vizuri ili niweze kufunga mabao mengi zaidi na kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri katika mechi zinazofuata,” amesema.