Polisi haicheki na yeyote Ligi Kuu Zanzibar
Muktasari:
- Kwa mantiki hiyo kila timu inapaswa kucheza kwa tahadhari zaidi kwani ikipoteza mechi moja tu inatoa nafasi kwa mpinzani wake kupanda.
POLISI imeendeleza rekodi ya kuwa timu pekee kwenye Ligi Kuu Zanzibar ambayo haijapoteza mechi yoyote msimu huu.
Katika mechi iliyochezwa Oktoba 30, 2026, timu hiyo iliifunga Black Sailors mabao 3-0 na Abdallah Kombo aliitangulizia dakika ya 23 na kuifanya kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Dakika ya 50, Salum Akida ameongeza la pili huku Kea Ramadhan akihitimisha kwa kufunga la tatu dakika ya 69.
Ushindi huo unaifanya Polisi kulinda rekodi yake ya kutopoteza kati ya mechi tisa ilizocheza timu hiyo iliyopo nafasi ya pili ya msimamo ikikusanya pointi 21, ikizidiwa moja na Zimamoto yenye 22 ikiwa kileleni.
Kati ya mechi tisa ilizocheza timu hiyo, imeshinda saba, sare tatu na kufunga mabao 13, ikifungwa matatu sawa na iliyofungwa KVZ iliyopo ya tano.
KVZ na Polisi ndizo pekee zilizofungwa mabao machache kwenye ligi hiyo hadi sasa kwa kuruhusu matatu kila moja, kabla ya jana KVZ haijacheza.
Mbio za ubingwa zimezidi kunoga baada ya timu zilizopo juu ya msimamo kupishana kwa pointi moja na JKU iliyopo nafasi ya tatu kabla ya mechi ya jana, ilihitaji ushindi kufikisha pointi 20.
Kwa mantiki hiyo kila timu inapaswa kucheza kwa tahadhari zaidi kwani ikipoteza mechi moja tu inatoa nafasi kwa mpinzani wake kupanda.