Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Premier Bet Tanzania yaendelea kutoa burudani, kumwaga mamilioni kwa Watanzania

Meneja wa Uendeshaji wa Premier Bet Tanzania, Sami Matar (wa pili kushoto) na Meneja wa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Amanda Kusila (kushoto) wakikabidhi mfano wa hundi ya Sh 96,522,760 kwa mshindi wa michezo ya kubahatisha Kelvin Donatus (wa tatu kushoto) mara baada ya kubashiri kwa usahihi michezo 10 ya mpira wa miguu kwa kiasi cha Sh 100,000. Wengine ni Afisa Mkaguzi Mkuu wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Emmanuel Ndaki (wa pili kulia) na Meneja Biashara wa Premier Bet Tanzania, Joy El Chwaifaty (kulia).

“Michezo ya Kubahatisha ni burudani sio ajira” ndiyo kauli unayoweza kuitumia katika kuelezea dhana nzima ya michezo ya kubahatisha ambayo kwa sasa imeshamiri sio Tanzania tu, bali Afrika na duniani kote.

Michezo ya kubahatisha imekuwa burudani kubwa ambayo mbali na kuwafanya watu wafurahi lakini pia imekuwa ikiwapatia vipato pale inapotokea mtu ameshinda ubashiri wake.

Mbali na vipato wanavyopata wachezaji wa michezo hiyo, lakini pia Serikali imekuwa ikipata mapato kutokana na kodi na tozo mbalimbali zinazolipwa na kampuni zinazoendesha michezo hiyo.

Premier Bet Tanzania kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri nchini, imekuwa chaguo la kwanza kwa wapenzi wa michezo ya kubahatisha nchini.

Hii ni kutokana na uwepo wa machaguo mengi ya michezo, rahisi kutumia, uaminifu katika kuwalipa walioshinda pamoja na weledi mkubwa wa kuendesha michezo yao.

Hii inatokana na timu imara ya wataalamu wenye weledi pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa za michezo ya kubahatisha kuanzia ile ya mtandaoni mpaka ya kwenye makaratasi.

Jana, Julai 21, 2023 kampuni hiyo ilikabidhi kitita cha Sh 96.52 milioni kwa mshindi wa michezo ya kubahatisha Kelvin Donatus  mkazi wa Arusha ambaye alibashiri mechi za mpira wa miguu.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi fedha hizo iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Uendeshaji wa Premier Bet Tanzania, Sami Matar amesema ushindi huo wa kipekee unaonyesha uwezo wa michezo ya kubahatisha kwenye kuleta mafanikio yanayobadilisha maisha.

Meneja wa Uendeshaji wa Premier Bet Tanzania, Sami Matar (wa pili kushoto) akipeana mkono na mshindi wa michezo ya kubahatisha Kelvin Donatus (wa tatu kushoto) mara baada ya kukabidhiwa pesa taslimu Sh 96,522,760. Wengine ni Meneja wa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Amanda Kusila (kushoto), Afisa Mkaguzi Mkuu wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Emmanuel Ndaki (wa pili kulia) na Meneja Biashara wa Premier Bet Tanzania, Joy El Chwaifaty (kulia).

“Tuko hapa kusherehekea ushindi mkubwa wa mmoja wa wateja wetu, Kelvin ambaye ni muongoza watalii kutoka Arusha, Tanzania aliyepata ushindi mkubwa na wa kushangaza katika ubashiri wa michezo. Hivi karibuni, Kelvin ameshinda kiasi cha Sh96,522,760 kutoka kwenye tiketi yake iliyokuwa na mechi 10, kwa dau la Sh100,000 tu,” amesema Matar.

Matar alimpongeza Kelvin kwa ushindi huo na kueleza kuwa mafanikio yake yanawapa hamasa wateja wote wa kampuni hiyo, kuonyesha kuwa ndoto zinaweza kutimia kwa wote wenye bahati na umakini kidogo kwenye kufanya machaguo ya michezo ya kubahatisha.

“Hata hivyo nasisitiza umuhimu wa kubashiri kistaarabu. Premier Bet Tanzania, tunajitahidi kuhamasisha sera ya kubashiri Kistaarabu kwa wateja wetu wote. Japokuwa kushinda kiasi kikubwa kama hicho ni jambo ambalo litawapa wengi hamasa, lakini lazima tukumbushane kuwa michezo ya kubahatisha lazima ifanywe kwa ustaarabu na watu wawe na uelewa mzuri wa hasara zinazohusika,” amesisitiza Matar.

Amesema lengo ni kuhakikisha kwamba kila mtu anayebashiri na Premier Bet Tanzania anapata jukwaa salama na la kufurahisha wakati wa kubashiri. “Tunafanya kazi kwa bidii kuhakikisha wateja wetu wanakuwa waadilifu na wawajibikaji wanapojishughulisha na michezo hii ya kubahatisha.”

Kwa upande wake Meneja wa Rasilimali Watu wa Premier Bet Tanzania, Amanda Kusila amesema wana furaha kubwa kuwa sehemu ya mafanikio ya Kelvin ambaye ameshinda kiasi hicho cha fedha kutoka kwenye mkeka wake uliokuwa na machaguo ya mechi 10 za mpira kwa dau la Sh100,000 tu. “Haya ni mafanikio ya kipekee na tunampongeza kwa ushindi wake huu mkubwa.” 

Meneja wa Rasilimali Watu wa Premier Bet Tanzania, Amanda Kusila (kushoto) akimkabidhi mshindi wa michezo ya kubahatisha Kelvin Donatus (wa pili kushoto) pesa taslimu Sh 96,522,760 ambaye alishinda kwa kubashiri michezo 10 ya mpira wa miguu kwa usahihi. Wengine ni Afisa Mkaguzi Mkuu wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Emmanuel Ndaki (kulia) na Meneja Biashara wa Premier Bet Tanzania, Joy El Chwaifaty (wa pili kulia).

“Tunajitahidi kuhamasisha sera ya kubashiri kistaarabu. Tunapenda wateja wetu waelewe kuwa kubashiri ni burudani na haitakiwi kugharimu afya ya mtu. Kwa sababu hiyo, tunasisitiza sana suala la kubashiri ksitaarabu na tumeweka hatua kadhaa ili kuhakikisha usalama na ustawi wa wateja wetu,” amesema Amanda.

Amesema moja ya mambo muhimu katika kubashiri kwa ustaarabu ni kuhakikisha kuwa huduma ya kubashiri inatolewa tu kwa wateja walio na umri halali. Kwa nguvu zote, wanakataza watu walio chini ya umri wa miaka 18 kushiriki katika michezo ya kubahatisha kwenye kampuni yetu.

Naye Afisa Mkaguzi Mkuu wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Emmanuel Ndaki amesema wao kama bodi wanahakikisha michezo ya kubahatisha inaendeshwa kwa kufuata sheria, washindi wanapatikana kwa haki kama ambavyo imepangwa na kile kilichoahidiwa kinatolewa.

“Pamoja na fedha ambazo washindi wanazipata kama ilivyotokea kwa Kelvin, bodi inaendelea kusisitiza kuwa michezo ya kubahatisha ni burudani kama zilivyo nyingine, wachezaji wacheze kwa kiasi kwa kutambua kwamba ukizidisha ina madhara,” amesema Ndaki.

Akizungumzia ushindi wake, Kelvin amesema ni jambo ambalo hakulitarajia kwani yeye alicheza tu kama sehemu ya burudani lakini akafanikiwa kushinda.

“Kushinda kiasi hiki kikubwa ni kama ndoto kwangu! Kama kijana ambae ni muongoza watalii, ninayejishughulisha na shughuli za kuwatembeza wageni maeneo yenye vivutio vya nchi yetu sikuwahi kufikiria kupitia Premier Bet Tanzania ningepata fursa hii ya kubadilisha maisha. Bila shaka hii bahati itanifungulia fursa nyingi mpya na kuniwezesha kuleta mabadiliko chanya katika jamii yangu,” amesema Kelvin.

Aliongeza kuwa, “Ushauri wangu kwa wenzangu wanaopenda michezo ya kubahatisha ni kubashiri kwa ustaarabu. Najua ushindi wangu ni hamasa lakini ni muhimu kutumia michezo hii kama burudani badala ya njia ya kujipatia fedha,”