Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Geita Gold azivaa Simba, Azam

CHIRWA Pict

Muktasari:

  • Simba ikiwa kwenye ubora wa hali ya juu juzi iliitandika Geita Gold mabao 2-0, wakiwa na muendelezo mzuri baada ya kushinda mechi tano za ligi kuu.

LICHA ya kushindwa kuifunga Simba, mshambuliaji wa Geita Gold Obrey Chirwa amesema wekundu hao wana nguvu kubwa eneo la kiungo pamoja na mawinga, jambo linaloweza kuwapa faida wanapokuwa na nafasi ya kushambulia au kulinda lango lao.

Simba ikiwa kwenye ubora wa hali ya juu juzi iliitandika Geita Gold mabao 2-0, wakiwa na muendelezo mzuri baada ya kushinda mechi tano za ligi kuu.

Chirwa mwenye mabao manne katika mechi tano alizoichezea Geita amesema Simba haijafikia kiwango cha kuonekana kuwa timu isiyoweza kufungika kama ilivyokuwa katika misimu iliyopita, huku akidai kuna maeneo ambayo wapinzani wanaweza kuyatumia kuwasumbua.

“Simba si ngumu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Wana ubora, lakini ukiangalia kikosi chao kuna maeneo ambayo unaweza kuyatumia. Sisi tumeshindwa kuwafunga, lakini tukikutana tena tutakuwa na nafasi ya kulipa kisasi,” amesema Chirwa.

CHIRW 01

Chirwa amesema mbali na ubora wa viungo, Simba inapata nguvu zaidi kupitia mawinga wake wenye kasi na uwezo wa kugeuza mchezo ndani ya muda mfupi.

“Simba ina nguvu zaidi eneo la kiungo na ina mawinga wenye kasi, hali hii inawapa wastani mzuri kwenye kulinda na kushambulia. Ukipoteza mpira na kuwapa nafasi ya kukimbia, wanaweza kukutesa, spidi hiyo haizuii kuwa miongoni mwa timu zisizofungika, lakini ni lazima timu yako ijitoe haswa” amesema.


CHIRW 02

AZAM HAINA UKUTA MGUMU

Akizungumzia Azam ambayo walicheza nayo na kuambulia sare ya mabao 2-2, Chirwa amesema hakubaliani na mtazamo, timu hiyo ina safu bora ya beki ambayo ni ngumu, huku akisema beki Twalib Nuhu ni mmoja wa wachezaji ambao wapinzani wanaweza kumtumia kama njia wanapokutana na Azam.

“Azam nao hawana ukuta mgumu sana. Kuna maeneo unaweza kuyatumia, hata Twalib Nuhu unaweza kumlenga ukiwa unataka kutengeneza nafasi ni swala la umakini wa hali ya juu na ubora ndio utakaosababisha mabao,” amesema.

Geita bado itasalia mjini ikiisubiri Yanga itakayovaana nayo Septemba 8, 2026 katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, kuanzia saa1:00 jioni.

Geita kwa sasa iko nafasi ya sita, baada ya mechi tano, imeshinda mbili, sare mmoja na kupoteza mbili ikiwa na pointi saba.