TFF yamfungia Jamal Bakhresa mwaka mmoja
Muktasari:
- “Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia Kiongozi wa Azam FC, Jamal Bakhresa kujishughulisha na mpira wa miguu kwa kipindi cha mwaka mmoja”.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kamati yake ya nidhamu imemfungia kiongozi wa Azam FC, Jamal Bakhresa kujihusisha na mpira wa miguu kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kumkuta na hatia kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu alivyofanya kabla na baada ya mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB iliyochezwa kisiwani Pemba.
Kupitia taarifa iliyotolewa na TFF imesema:
“Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia Kiongozi wa Azam FC, Jamal Bakhresa kujishughulisha na mpira wa miguu kwa kipindi cha mwaka mmoja”.
“Bakhresa ametiwa hatiani kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu alivyofanya kabla na baada ya mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB iliyochezwa kisiwani Pemba”.
“Mlalamikiwa alikiri kufanya makosa mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Wakili Alex Mushumbusi kwa malalamiko yote mawili yaliyowasilishwa dhidi yake”.
“Aliomba radhi kwa TFF kwa makosa aliyofanya, na kuahidi kutorudia tena”.
“Kamati ilimtia hatiani kwa kuzingatia Ibara ya 11(f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF, Toleo la 2021”.