Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Transit Camp yamrejesha Lyakuka

MAAFANDE Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wa Lyakuka amerejea tena ndani ya kikosi hicho baada ya kukifundisha pia mara ya mwisho msimu wa 2023-2024 na kumaliza nafasi ya 13 na pointi zake 27, kufuatia kushinda mechi sita, sare tisa na kupoteza 15, kati ya 30, iliyocheza.

UONGOZI wa maafande wa Transit Camp, umemrejesha tena kocha mkuu wa timu hiyo, Said Lyakuka kwa ajili ya kukifundisha kikosi hicho kwa msimu huu wa 2026-2027, wa Ligi ya Championship, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Vicent Barnabas.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Transit Camp, Hassan Udda, amesema baada ya kuondoka Barnabas wamefikia makubaliano ya kumrejesha tena Lyakuka, wakiamini uzoefu wake katika kikosi hicho utaleta pia matokeo chanya.

“Ni kocha mzoefu na anaijua vizuri Transit Camp, tumefikia makubaliano hayo baada ya mchakato wa muda mrefu wa kumtafuta mbadala wa Barnabas, malengo yetu ni kuhakikisha timu inacheza Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wa 2027-2028,” amesema Udda.

Barnabas alijiunga na timu hiyo Februari 27, 2026, akichukua nafasi ya Kocha, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’, aliyejiunga na Tanzania Prisons, ambapo kwa msimu wa 2025-2026, alikiwezesha kikosi hicho kumaliza kikiwa nafasi ya tano na pointi 56.

Kwa upande wa Lyakuka amerejea tena ndani ya kikosi hicho baada ya kukifundisha pia mara ya mwisho msimu wa 2023-2024 na kumaliza nafasi ya 13 na pointi zake 27, kufuatia kushinda mechi sita, sare tisa na kupoteza 15, kati ya 30, iliyocheza.