Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yashindwa kufurukuta, Simba ikiendeleza ubabe

YANGA P Pict

Muktasari:

  • Yanga Princess ambayo ilikuwa nyumbani Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, imekubali kichapo hicho kwa bao la dakika ya 36 lililofungwa na mshambuliaji Asha Mwalala akimalizia mpira uliopigwa na Neema John.

NDIO hivyo kama mlivyosikia! Yanga Princess imeshindwa kufurukuta mbele ya JKT Queens baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, huku mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania Bara, Simba Queens ikiitandika Mashujaa Queens mabao 2-0 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Yanga Princess ambayo ilikuwa nyumbani Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, imekubali kichapo hicho kwa bao la dakika ya 36 lililofungwa na mshambuliaji Asha Mwalala akimalizia mpira uliopigwa na Neema John.

Katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Mzee, Dar es Salaam, Simba Queens imeendeleza ubora wake kwa kuichapa Mashujaa Queens 2-0, mabao yaliyofungwa na Vivian Corazone na Zainah Nandede.

YANG 01

Kwa upande wa Yanga Princess na JKT Queens, mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kila timu ikitawala vipindi tofauti ambapo JKT ilikuwa bora dakika 45 za kwanza na Yanga ikitawala kipindi cha pili.

Kabla ya bao hilo, Anastazia Katunzi aliifungia JKT kwa mpira wa adhabu dakika ya 14, lakini mwamuzi alilikataa akitafsiri kuwa kulikuwa na tukio la kuotea.

Yanga ilipata nafasi ya kusawazisha dakika ya 45 kupitia Salamata Kouanda, lakini bao lake pia lilikataliwa kwa sababu ya kuotea. 

Ushindi huo ni muhimu kwa JKT Queens kutokana na ushindani uliopo katika nafasi za juu. Timu hiyo ilikuwa imeanza msimu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Queens na Bunda Girls, kabla ya kuiongezea Yanga Princess kipigo hicho cha bao 1-0.

YANG 02

Kwa upande wa Simba Queens, ushindi dhidi ya Mashujaa Queens unaifanya iendelee na mwanzo mzuri wa msimu baada ya awali kuifunga Kilimanjaro Wonders mabao 3-0 na Fountain Gate Princess bao 1-0. Hivyo, Simba na JKT zimefikisha pointi tisa kila moja baada ya raundi tatu, huku Yanga Princess ikiwa nazo sita.

Matokeo ya mechi nyingine za mzunguko wa tatu, Alliance Girls ikiwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, imetoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bunda Queens, Bunda Girls imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Queens, Ceasiaa Queens imeitandika Tausi FC mabao 2-0 na Kilimanjaro Wonders ikitoka suluhu dhidi ya Fountain Gate Princess.