Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar Old Stars yajinoa

Muktasari:

  • Ziara hiyo ililenga kujionea maandalizi ya kikosi hicho kinachojifua kabla ya kutimkia Kenya kushiriki mashindano ya wachezaji wa zamani yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini humo.

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Hussein Ahmada, akiambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango wa ZFF, Awadh Maulid, wamewatembelea wachezaji wa zamani wa Zanzibar maarufu Zanzibar Old Stars katika viwanja vya Mambosasa kisiwani Unguja.


Ziara hiyo ililenga kujionea maandalizi ya kikosi hicho kinachojifua kabla ya kutimkia Kenya kushiriki mashindano ya wachezaji wa zamani yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini humo.

Akiwasilisha salamu za shirikisho hilo, katibu huyo amesema ZFF itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati na kuwa karibu na timu hiyo muda wote kwani inathamini juhudi zao.

Ahmada amesisitiza kuwa, ZFF inatambua na kuthamini uwepo wa wachezaji hao kwa sababu uzoefu wao bado ni nguzo muhimu katika kuuendeleza na kuulea mchezo wa mpira wa miguu kisiwani hapa.

Pamoja na mambo mengine, ZFF imewakabidhi wachezaji hao vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya kufanya mazoezi na maandalizi ya kushiriki mashindano hayo, hatua iliyopokelewa kwa furaha kubwa na kikosi chote cha Zanzibar Old Stars.

Mbali na vifaa hivyo vya michezo, ZFF pia imewakabidhi fedha wachezaji hao ili kusaidia kugharamia mahitaji mbalimbali ya maandalizi ya safari hiyo.

“Nyinyi ni wachezaji nguli ambao mliwahi kupeperusha vyema bendera ya Zanzibar katika miaka ya nyuma na mmeonesha nia ya dhati ya kupambana kwa lengo la kurudi na ushindi nyumbani ili kuendeleza heshima ya soka la Zanzibar,” amesema Ahmada.