Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZSSF yakabidhi Uwanja wa Malindi

ZFF Pict

Muktasari:

  • Uwanja huo ambao awali lilikuwa eneo la wazi, kwa sasa umefanyiwa maboresho makubwa na kuwa uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa utakaotumika kwa mazoezi na mechi za mashindano mbalimbali.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema kukabidhiwa kwa Uwanja wa Malindi ni miongoni mwa juhudi za Serikali kuhakikisha vipaji vinaendelezwa.

Ameyasema hayo wakati wa makabidhiano wa uwanja wa mpira wa mgiuu kati ya Wizara hiyo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), yaliyofanyika eneo la Malindi, Mjini Unguja.

Amesema uwanja huo utatoa fursa na nafasi kwa watoto na vijana kuendeleza kukuza vipaji vyao katika michezo.

Alieleza wizara hiyo inashirikiana na wadau wa soka wakiwemo ZSSF ili kuhakikisha uwanja huo unakuwa kwenye mazingira mazuri.

Pia, aliitaka ZSSF kuendelea kuwa mshirika muhimu wa michezo kukabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza kwa wanamichezo, jambo ambalo litasaidia kuendeleza vipaji vyao.

"Naisihi ZSSF kuwa mshirika muhimu wa kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza kwa wanamichezo hao," amesema.

Vilevile, aliifahamisha ZSSF kwamba ni vyema timu ya wataalamu wa pande zote mbili kushirikiana pamoja na kuweka utaratibu mzuri juu ya utumiaji wa viwanja hivyo.

Mkurugenzo wa mfuko huo, Nassor Shaaban Ameir amesema kukamilika kwa uwanja huo utasaidia kuwawezesha vijana kucheza mpira sehemu rafiki.

Amesema mfuko huo umekuwa mstari wa mbele kuunga mkono maono ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi katika kuboresha miundombinu ya michezo.

Uwanja huo ambao awali lilikuwa eneo la wazi, kwa sasa umefanyiwa maboresho makubwa na kuwa uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa utakaotumika kwa mazoezi na mechi za mashindano mbalimbali.