Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bado pointi moja Liverpool kutwaa bingwa EPL

Muktasari:

  • Liverpool inahitaji pointi moja kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Crystal Palace, Arsenal imejikuta ikiipunguzia Liverpool idadi ya pointi zilizobaki kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Katika mchezo wa jana Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya tatu kupitia Jakub Kiwior ambaye alimalizia kwa kichwa krosi ya Martin Ødegaard.

Eberechi Eze aliifungia Crystal Palace bao la kusawazisha dakika ya 27, kisha Leandro Trossard akaiweka tena mbele Arsenal kwa bao la dakika ya 42 na kufanya kwenda mapumziko Arsenal ikiongoza 2-1.

Dakika ya 83, Jean-Philippe Mateta aliisawazishia Crystal Palace na kufanya matokeo kuwa sare ya 2-2 hadi mwisho wa mchezo.

Baada ya mchezo huo, Arsenal imefikisha pointi 67 ikiwa nyuma ya vinara wa ligi Liverpool yenye 79, tofauti yao ikiwa ni pointi 12.

Hadi sasa Arsenal imebakiza michezo minne kukamilisha ratiba ya ligi msimu huu ikiwa imecheza michezo 34 ambapo imeshinda mechi 18, sare 13 na kupoteza tatu.

Kwa upande wa Liverpool, imecheza mechi 33, imeshinda 24, sare saba na kupoteza mbili. Kwa sasa timu hiyo inahitaji pointi moja katika mechi tano zilizobaki ili kutangaza ubingwa msimu huu kwani pointi 80 zitaifanya kutofikiwa na nyingine kwenye ligi hiyo.

Iwapo Liverpool itapata ushindi au sare kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Tottenham utakaochezwa Jumapili hii Aprili 27, 2025, majogoo hao wa Anfield watatangaza ubingwa wakiwa nyumbani.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot huenda akaingia kwenye rekodi ya makocha waliowahi kutwaa taji la Ligi Kuu England katika misimu yao ya kwanza kama walivyofanya Jose Mourinho (Chelsea) msimu 2004-2005, Antonio Conte (Chelsea) msimu 2016-2017, Carlo Ancelotti (Chelsea) msimu 2009-2010 na Manuel Pellegrini (Manchester City) msimu 2013-2014.