Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Bruyne mawazo yote Marekani

Muktasari:

  • De Bruyne, 33, sasa anatazama hatima ya maisha yake ya soka baada ya mkataba wake kubakiza miezi michache kufika tamati na utamalizika mwishoni mwa msimu huu.

NOTTINGHAM, ENGLAND: KIUNGO Kevin De Bruyne ameweka wazi mipango yake ya kuachana na Manchester City huku uliopo mezani ni kwenda kujiunga na klabu ya San Diego ya Ligi Kuu Marekani, imeelezwa.

De Bruyne, 33, sasa anatazama hatima ya maisha yake ya soka baada ya mkataba wake kubakiza miezi michache kufika tamati na utamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo wa Kijerumani ametumikia Man City kwa muongo mmoja kwenye kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi Kuu England, lakini sasa atalazimika kuhama mkataba wake utakapofika tamati Juni 30.

De Bruyne ana ofa kibao nono tu mezani kwake kutoka Saudi Arabia, lakini kinachoripotiwa, anavutiwa na mpango wa kwenda kukipiga Marekani endapo kama ataamua kuachana na Man City.

San Diego, ambayo itacheza Ligi Kuu Marekani kwa mara ya kwnaza ni moja ya timu zinazovutiwa na De Bruyne.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola alizungumzia ishu ya hatima ya mchezaji De Bruyne mwezi uliopita, akisema staa huyo mwenye umri wa miaka 33 ataamua mwenyewe hatima yake.

"Hakuna kitakachokwenda kubadilika juu ya hilo. Bila shaka jambo hilo linafahamika na mwenyewe atakuwa na uamuzi," alisema Guardiola.

"Nadhani ni kitu atakachotakiwa kufanya uamuzi, ambacho ni muhimu kwake. Anapaswa awe mkweli tu yeye mwenyewe ni kitu gani atakwenda kufanya katika maisha yake. Atafikisha umri wa miaka 34 itakapofika mwisho wa msimu na hapo atalazimika kufanya uamuzi, kama ilivyotokea kwa David Silva."

Man City mechi yao ijayo watakipiga na Bournemouth kwenye robo fainali ya Kombe la FA.