Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kounde mguu sawa Arsenal

Muktasari:

  • Beki huyu mwenye umri wa miaka 26, ameingia katika rada za Arsenal ikiwa ni katika mpango wa benchi la ufundi la timu hiyo katika kuweka mambo sawa eneo la ulinzi.

ARSENAL wanapanga kuwasilisha ofa ya Pauni 55 milioni katika timu ya Barcelona kwa ajili ya kuipata saini ya beki kisiki wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ufaransa, Jules Kounde.

Beki huyu mwenye umri wa miaka 26, ameingia katika rada za Arsenal ikiwa ni katika mpango wa benchi la ufundi la timu hiyo katika kuweka mambo sawa eneo la ulinzi.

Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Arsenal inataka kumsajili supastaa huyo ili akawe mbadala sahihi wa William Saliba anayeweza kuondoka mwisho wa msimu huu kujiunga na Real Madrid ambayo imeanza kumfuatilia kwa muda mrefu.

Mbali ya kucheza kama beki wa kulia mara nyingi, mchezaji huyo pia ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati, ingawa mara kwa mara hucheza pembeni, akiwa na sifa kubwa ya kupandisha mashambulizi.

Mkataba wa sasa wa Kounde unatarajiwa kumalizika 2027


Aaron Ramsdale

MANCHESTER United bado wana mpango wa  kumsajili kipa wa Southampton, Aaron Ramsdale mwenye umri wa miaka 26, ambaye ameanza kutafuta timu baada ya Southampton kushuka daraja hivi karibuni. Mabosi wa Manchester United wanataka kumsajili staa huyou kutokana na kiwango cha kipa wao wa sasa, Andre Onana. Mkataba wa Ramsdale unatarajiwa kumalizika 2028.


Georginio Rutter

CHELSEA wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa Brighton na Ufaransa, Georginio Rutter ambaye inataka kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi. Rutter ameingia kwenye rada za Chelsea baada ya msimu huu kuonyesha kiwango bora akicheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao manane.


Thomas Partey

ATLETICO Madrid wameachana na mpango wa kutaka kumsajili  kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Ghana, Thomas Partey, 31. ambaye mkataba wake na Arsenal unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Partey alikuwa akihusishwa kuondoka awali lakini sasa Arsenal wameshaanza mazungumzo na wawakilishi wake kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya.


Caoimhin Kelleher

WEST Ham United wanataka kumsajili kipa wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland, Caoimhin Kelleher mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha la majira ya kiangazi. Kelleher anataka kuondoka Liverpool kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Majogoo. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2026.


Tammy Abraham

AC Milan inataka kumsainisha mkataba wa kudumu straika wa AS Roma, Tammy Abraham, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuridhishwa na kiwango alichoonyesha tangu ajiunge kwa mkopo msimu huu. Mbali ya AC Milan kwa upande mwingine, Roma pia inataka kumsainisha mkataba wa kudumu kiungo wa AC Milan na Ubelgiji Alexis Saelemaekers, 25, ambaye anacheza kwa mkopo katika kikosi hicho.


Xavi Simons

MANCHESTER United wanafikiria kumgeukia mshambuliaji wa RB Leipzig, Xavi Simons, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa dili la kumsajili straika wa Wolves na timu ya taifa ya Brazil, Matheus Cunha, 25, litashindikana. Kocha wa Mashetani Wekundu, Ruben Amorim kipaumbele chake cha kwanza ni kumsajili Cunha.


Antony

REAL Betis imetuma maombi ya kumsajili tena kwa mkopo wa msimu mzima mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil, Antony, 25, ambaye anacheza kwa mkopo katika kikosi hicho kwa sasa. Antony ambaye ni mmoja kati ya mastaa waliokuwa hawapati nafasi ya kutosha Manchester United, mkataba wake na timu hiyo unatarajiwa kuisha 2027.