Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Bruyne: Ubora kwanza, mkataba sijali

Kelvin Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Kibelgiji, De Bruyne, 33, mkataba wake utamalizika mwisho wa msimu na amekuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na mabingwa hao wa Ligi Kuu England. Hatima yake haijafikiwa mwafaka juu ya mkataba mpya, kwa sababu bado hajasaini mkataba wa kubaki Manchester.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO, Kevin De Bruyne amesema akili yake kwa sasa imewekeza kwenye kurudisha ubora wa soka lake kuliko kufikiria maisha yake yajayo kwenye kikosi cha Manchester City.

Kiungo huyo wa Kibelgiji, De Bruyne, 33, mkataba wake utamalizika mwisho wa msimu na amekuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na mabingwa hao wa Ligi Kuu England. Hatima yake haijafikiwa mwafaka juu ya mkataba mpya, kwa sababu bado hajasaini mkataba wa kubaki Manchester.

De Bruyne amekosa mechi kibao msimu huu kutokana na maumivu ya misuli, lakini ameanzishwa kwenye mechi mbili zilizopita, ambazo zote Man City ilipata ushindi. Na amedai kwamba anachopambania kwa sasa ni kurudi kwenye ubora wa soka lake na si ishu ya hatima ya maisha yake Etihad.

Alipoulizwa kuhusu mkataba mpya Man City baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya West Ham, De Bruyne alisema: “Wala sijali.

“Ninachojaribu kwa sasa ni kurudi kwenye ubora wangu. Ninachokiona kila wiki narudi kwenye ubora mzuri. Kwenye hali ya utimamu nazidi kuimarika na naweza kukimbia kwa dakika 90 sasa. Nilikuwa sijisikii vizuri kwa miezi kadhaa nyuma kutokana na kuwa maumivu, lakini sasa naendelea vizuri.”

De Bruyne alionekana kuirudisha Man City kwenye ubora wake katika mechi ambayo Erling Haaland na Phil Foden wote walifunga mabao. Man City sasa imeshinda mechi mbili mfululizo huku Haaland na Foden walitupia nyavuni, huku De Bruyne akipata nafasi ya kucheza kwa mechi ya pili.

Kiungo huyo Mbelgiji amekuwa kwenye kiwango bora cha Man City kwa miaka tisa, lakini siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na mpango wa kutimkia Marekani. Na hilo limekuja baada ya Pep Guardiola kudai kwamba ishu ya kumwongezea mkataba De Bruyne hiyo haimuhusu.